Kasisi mwenye utata Ng’ang’a ameelezea maoni yake kuhusu kutimuliwa kwa Mawaziri na Rais hapo jana.
”Leo nataka niongee kwa kiingereza kwa sababu rafiki yangu, CS wa usafiri umeenda nyumbani. Nilikuambia utakabiliana na matokeo. Hata, ninakuja nyuma yako. Naapa mbele za Mungu, nitawapinga.”
Ng’ang’a alimshukuru rais kwa hatua yake ya kuwafuta kazi mawaziri.
"Asante Mheshimiwa kwa kuwafuta kazi watu hawa." Alisema.
Pia alishangaa kwamba mawaziri wote walifutwa kazi na kusema kuwa angepatana na Rais angemnunulia chai.
“Leo Rais ningekupata kwa duka ningenunulia cha lakini nivile siwezi kupata.”
Ng’ang’a alisema kwamba Rais alifanya Jambo la maana Kwa sababu wengi walikuwa awafanyi kazi yao na walifanya serikali ionekane kwamba iko na makosa.
Jana, Rais Ruto alikubali shinikizo la Gen Z na kuamua kuwasikiliza kwa kuwafuta kazi makatibu wa baraza la mawaziri.
Rais William Ruto amelivunja Baraza lake la Mawaziri na kuwarudisha nyumbani mawaziri wote na mwanasheria mkuu.
Uamuzi huo hauathiri Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.
"Nimeamua kuwafuta kazi mara moja mawaziri na mwanasheria mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya isipokuwa waziri mwenye mamlaka makuu na Katibu wa Baraza la Mawaziri," Ruto alisema.
"Na bila shaka, afisi ya Naibu Rais haiathiriwi kwa vyovyote vile."
Rais alisema mambo ya Wizara kuanzia sasa yataratibiwa na Makatibu Wakuu hadi baraza la mawaziri litakapoteuliwa.
Mkuu wa Nchi alisema baraza jipya la mawaziri litatajwa baada ya mashauriano ya kina katika sekta zote