logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mrembo alia kwa furaha kuona wazazi wake wakirudiana baada ya kutengana kwa miaka 30

Walionekana kwenye studio ya picha huku wakipiga pozi tofauti kusherehekea kuungana kwao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani15 July 2024 - 13:56

Muhtasari


  • • Katika video hiyo, wanandoa hao ambao wametengana kwa miaka 30, wanaonekana wakitabasamu na kukumbatiana, wakisherehekea kuungana kwao na binti yao.
  •  
WANANDOA WARUDIANA BAADA YA KUACHANA MIAKA 30

Video ya kuchangamsha nyoyo inayoendelea kusambaa mtandaoni imenasa wakati wa kupendeza ambao wanandoa wazee waliungana tena baada ya kutengana kwa miongo mitatu na kwa muda mrefu, iliwachangamsha watu wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video iliyochapishwa na binti yao, @debbienes kupitia TikTok, mwanamume huyo alionekana akiwa amevalia mavazi meupe yanayolingana na mkewe, kuonyesha uhusiano wao wa karibu.

Walionekana kwenye studio ya picha huku wakipiga pozi tofauti kusherehekea kuungana kwao.

Picha hizo zinaonyesha pozi mbalimbali, zikiwemo picha kadhaa za kupendwa za wanandoa walioungana tena na nyingine wakiwa na mwanao huyo.

Katika video hiyo, wanandoa hao ambao wametengana kwa miaka 30, wanaonekana wakitabasamu na kukumbatiana, wakisherehekea kuungana kwao na binti yao.

Mrmbo huyo alinukuu video hiyo akisema “Wazazi wako waliungana pamoja tena baada ya miaka 30 ya kutengana.” Kisha akaiambatanisha na wimbo unaosema “nilikuwa namtafuta Mungu, nilikuwa natafuta, ghafla nikakupata wewe, na niliamini kwamba ulikuwa kutoka kwa Mungu…”

Video hiyo ilipata mvuto haraka mtandaoni huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakitoa maoni yao kuhusu mapenzi yao mapya. Baadhi ya majibu yanaonyeshwa hapa chini:

Debo wa Lagos👸 alisema, "Naweza kusimulia    Yangu imetenganishwa kwa kama miaka 2 sasa na inaonekana kama milele".

chiefsdaughter__ alisema, "Wazazi wangu kuungana tena ilikuwa moja ya sehemu tamu zaidi ya maisha yangu lakini baba yangu alikufa baadaye😌lakini nina furaha walifanya kurudiana kabla hajaondoka".

VA_WuraolaA alisema, "Wow hii ilinifanya nitokwe na machozi…..Natamani baba yangu arudi pia, ingawa mama yangu hasemi lakini siwezi kufikiria jinsi atakavyokuwa mpweke".


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved