Msanii kutoka leob ya muziki ya WCB Wasafi, Zuchu amefunguka kwamba wimbo wake wa ‘Utaniua’ ambao aliutoa mwezi Mei mwaka jana ulikuwa ni hadithi ya kweli.
Zuchu, alifichua haya wakati alikuwa anatumbuiza kwenye hafla moja siku tatu zilizopita ambapo alikuwa anaimba acapella ya wimbo huo kwa raha za mashabiki waliokuwemo.
Baada ya kuimba aya ya kwanza, Zuchu alisitiza na kusema kwamba wazo la wimbo huo lilizaliwa kutokana na matukio ya kweli ambayo alikuwa ameyapitia kwenye mapenzi kipindi hicho, akisema kwamba alishikikwa hadi akashikika kimapenzi.
“Yooh, wimbo huo ulikuwa ni hadithi ya kweli, niwaambie tu. Nilishikwa nikashikika! Unajua yale mapenzi mazuri yanayopitia mpaka kwenye mishipa unaandika wimbo tu. Huu wimbo ulikuwa ni dedication kwa mtu Fulani wa maana sana kwangu,” Zuchu alisema kabla ya kuendelea kuimba.
Wimbo huo ulitoka Mei 2023 na kufikia sasa umejizolea utazamaji mara milioni 21 kwenye YouTube.
Wimbo huo kwa sehemu unaimba;
Nina hamu mwenzenu nna hamu kuyahadithia, Oh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia Utanii kama utani, Tulianza kimasiara, Sikudhani sikudhani, Yatafikia mahala Akiwa hapatikani hapaliki, Sijalala, Kanifanya kitu gani, Mbona imekua mara Dua La kuku menipata mwewe Wallahi nyinyi ni mtihani, Hata makosa ayafanye yeye mimi ndo naomba samahani
Ona anacheka kama mazuri, Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli Eti kumwacha naanzaje asa kusepa natoa wapi jeuri, Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufulii