logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kabuda aeleza jinsi alivyopata wakati mgumu kuelewa masomo katika shule ya upili

Kabuda aliendelea zaidi kwa kutaja masomo ambayo yalikuwa yanampa wakati mgumu kuelewa kama hesabu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 July 2024 - 12:54

Muhtasari


  • •Kabuda aliendelea zaidi kwa kutaja masomo ambayo yalikuwa yanampa wakati mgumu kuelewa kama hesabu.
  • •Kabuda alisema kuwa somo alilolipenda sana katika shule ya upili ni CRE akisema ni somo ambalo alifanikiwa sana.

Mtayarishaji wa maudhui Kabuda amefunguka jinsi alivyokuwa akijitahidi kuelewa masomo katika shule ya sekondari.

Mcheza densi huyo alifichua wazi jinsi alivyokuwa akihangaika kuelewa masomo fulani alipokuwa shule ya upili.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Obinna, Kabuda alikiri wazi kwamba hakuwahi kupenda sana shule ya sekondari kwa sababu alikuwa akipata wakati mgumu  kujaribu kufanya mambo kwa kadiri ya taaluma yake.

“High school nilikua tuh sikua nashikanisha kitu chuo nilikua naona tuh Dim Dim tuh.” Kabuda alifichua.

Kabuda aliendelea zaidi kwa kutaja masomo ambayo yalikuwa yanampa wakati mgumu kuelewa.

“Huskii ni Mao, Chem kwanza Mao hiyo ilikua ngori sijui A+=Z aje surely!!!” kabuda alieleza.

Aliendelea kueleza jinsi alivyokatishwa tamaa, hasa kwa hisabati iliyohusisha hesabu ngumu, jambo ambalo siku zote halikuwa sawa naye.

Kabuda alisema kuwa somo alilolipenda sana katika shule ya upili ni CRE akisema ni somo ambalo alifanikiwa sana.

“Nilikuanga Genje kwanza CRE, mahali nilikua nakula mawe nje bado ilikua composition na Insha… Handwriting pia nilikua nyuma,” Kabuda alieleza.

Kabuda alipoulizwa mwalimu wake alikuwa akimpenda sana wakati alikuwa shule angeweza kutaja mmoja hii inaonyesha kuwa alikuwa na wakati mgumu shuleni.

“Paragasha, hata siwezi wakumbuka majina’ alieleza.

Kabuda alieleza kuwa licha ya mambo hayo amejitahidi sana kufika mahali alipo kwa sasa na kurudisha sifa zote kwa Mungu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved