Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amejizolea umaarufu mkubwa zaidi kuwa hi kushuhudiwa ndani ya siku moja baada ya kutambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Real Madrid nchini Uhispania.
Kabla ya utambulisho wake Jumanne, Mbappe alikuwa na wafuasi milioni 119 kwenye ukurasa wake wa instagrma lakini saa kadhaa baada ya kutambulishwa mbele ya umati wa mashabiki 80k, Instagram ya Mbappe ilivutia wafuasi wapya na kufikisha jumla ya wafuasi milioni 120.
Nahodha huyo wa Les Blues mwenye umri wa miaka 25 aliondoka Paris Saint Germain kwa uhamisho wa bure ili kutimiza ndoto zake za utotoni za kuichezea Real Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga na wababe hao wa Uhispania kwa mkataba wa miaka mitano, baada ya kuondoka Paris Saint Germain bila malipo baada ya miaka 6.
Mbappé alitumia mitandao ya kijamii kueleza kufurahishwa na "ndoto iliyotimia" huku nahodha huyo wa Les Blues akijiandaa kuliongoza taifa lake kwenye kipute cha kombe la dunia 2026.
Itakumbukwa pia mwezi mmoja uliopita, Ndani ya saa moja baada ya tangazo rasmi la uhamisho, nyota huyo wa Ufaransa alipata wafuasi wapya milioni 1.
Ndani ya saa nne zilizofuata, Mbappé alipata wafuasi wengine milioni 1, kuchukua wafuasi wake wa Instagram kutoka milioni 114 kabla ya kutangazwa hadi milioni 116 na kuhesabu, baada ya tangazo hilo.