logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Edwin Sifuna akiri kupokea jumbe nyingi kutoka kwa warembo

Nambari ya simu ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ilisambaa kwenye mtandaoni wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 July 2024 - 06:54

Muhtasari


  • •Edwin Sifuna anakiri kwamba wanawake wamekuwa wakimtumia ujumbe baada ya nambari yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
  • •Katibu Mkuu wa ODM alifichua kuwa alipokea jumbe nyingi kutoka kwa wasichana wadogo.
  • •Nambari ya simu ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ilisambaa kwenye mtandaoni wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna majuzi alijipata katika hali isiyotarajiwa baada ya nambari yake ya simu kufichuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Edwin Sifuna ni miongoni mwa viongozi ambao nambari zao za simu zilifichuliwa licha ya kutounga mkono Mswada wa Fedha wa 2024.

Akiongea wakati wa mahojiano katika Mic Cheque podcast, Edwin Sifuna alikiri kwamba kuna watu wabaya wanaojaribu kukashifu watu mashuhuri ambao wamejitahidi kujijenga.

Seneta wa Nairobi, ambaye alilazimishwa kushiriki kile msichana mmoja alimtumia, alisema kuwa huo ulikuwa ujumbe ambao hakuwahi kutarajia kupata.

“Wacha niwasomee moja, watu wameharibika bana, kuna dem anaitwa Ivy, mimi namwanika tu leo zile vitu watu wananiambia hapa kwa inbox. Hi, my name is Ivy Nimesikia, and you have been chewing on girls like nobody’s business."

"My only concern is where I can get the form so that I can sign up to volunteer.” Sifuna alisoma ujumbe huo.

Sifuna alichukua tukio hilo kwa mzaha, huku akiwashukuru kwa utani wale waliovujisha nambari yake.

Wale walikua wanashare number yangu wanadhani wananiumiza mnanijenga mbaya… Ile kitu naeza ambia Ivy, line ni mrefu lakini inasonga.” 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved