logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kanyari asema hawezi kuoa mwanamke ambaye atakuwa mzigo kwake

Kanyari alishiriki kuwa anataka mwanamke ambaye angeweza kujenga naye maisha huku wakisaidiana.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 July 2024 - 10:15

Muhtasari


  • •Mchungaji Kanyari alikuwa akihubiri alipoeleza kwamba yeye si kijana tena na kuorodhesha sifa bora alizotaka kwa mke.
  • •Mchungaji Kanyari alieleza kuwa anataka mwanamke ambaye angeweza kujenga naye maisha huku wakisaidiana.
MCHUNGAJI VICTOR KANYARI

Mchungaji Kanyari amefunguka kuhusu mwanamke  bora na kueleza kuwa anataka mke ambaye wanaweza kusaidiana naye.

Mchungaji Kanyari alikuwa akitoa mahubiri kanisani aliposhiriki kuwa hana nia ya kuoa mtu ambaye atakuwa mzigo maishani mwake.

“Siwezi kuona na mtu ambaye atakuwa mzigo maishani mwangu, hakuna faida yoyote unayoniletea zaidi ya kuwa mweupe.”

“Siwezi kukubali hivyo kazi yako itakuwa ya kuombaomba kwa watu mimi na wewe mimi ni mzee, mimi si kijana nataka mtu ambaye tunaweza kusaidiana."

 Kanyari pia alitoa mfano wa hali ambayo anaweza kuhubiri katika ibada ya kwanza huku mke wake akihubiri katika ibada ya pili.

Mchungaji Kanyari alisema mke wake anaweza kuwa anaendesha kanisa lao katika nchi tofauti, na yeye akifanya hivo Kenya.

 "lazima tunasaidiana," alisema.

Hivi majuzi Pasta Victor Kanyari aliwasisimua Wakenya kwa mara nyingine baada ya kutoa maoni yenye utata kuhusu aina ya wanawake ambao si wazuri katika kuwa wake.

Alifanya hivi kwenye ukurasa wake maarufu waTikTok ambapo alianza kwa kusema kuwa wanawake wanaozungumza Kiingereza sio wake na hawawezi kuwa wake wazuri.

"Kubali ukatae! Wife material haongeangi kizungu. Kama naongea uongo niambie! Nakama naongea ukweli andika hapo kwa comments, 'Prophet uko on point,'" alisema kwa imani kubwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved