Seneta maalum Karen Nyamu amezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba ana vidokezo muhimu vya kuwafanya wanaume kuwatambua wanawake wakweli.
Kupitia Instagram yake, Nyamu alisema kwamba ikiwa mwanamume anataka kumtambua mrembo wa kweli, si yule anayehitaji vitu vingi.
Kwa mujibu wa seneta huyo, mrembo wa kweli hawezi muomba mpenzi wake kitu chochote zaidi ya chakula na muda wake tu basi!
“Wasichana wakweli huwa hawahitaji kitu chochote zaidi isipokuwa chakula, muda wako na attention yako,” Nyamu alichapisha akiambatanisha na picha yake.
Hata hivyo, baadhi ya wanaume walimpinga vikali wakisema kwamba warembo wengi hata kama hawasemi kuwa kila mmoja anapoingia kwenye penzi lengo ni kupata matunzo bora kwa kutumia pesa, hilo huwa ndilo liko juu kwenye maazimio yao.
“Hamsemi Pesa but it's top on the list” Brian si Brayo
“🙌🙌The first time I have seen a girl not mentioning money on such situations 😂” mwingine alisema.
“Umeacha mapenzi hapo kwa hizo vitu za kupenda” wash victor.
Mwanasiasa huyo amekuwa akivutwa mitandaoni katika siku za hivi karibuni kisa msimamo wake kuhusu mswada ulioangushwa wa kifedha 2024.
Nyamu hadi alipeleka lalama zake kwenye bunge la seneti wiki chache zilizopita akidai kutukanwa vibaya mtandaoni na hata kupoteza wafuasi zaidi ya elfu 10 kwenye mtandao wa Instagram.