Babajide Israel Adebanjo, mwanamume kutoka Nigeria ametajwa kuwa ndiye anayeshikilia muda mrefu zaidi wa kutingisha kiuno (twerking) kwa mtu mmoja mmoja.
Israel alicheza kwa saa tatu na dakika thelathini mnamo Januari 14, 2024.
Miezi kadhaa baadaye, Rekodi ya Dunia ya Guinness ilimtangaza kama mmiliki wa taji kwa muda mrefu zaidi wa kutingisha kiuno.
The Guinness World Record ilieleza kwenye tovuti yake kuwa; "Jaribio hili la rekodi lilikuwa la kibinafsi kwa Babajide kwani ilikuwa njia yake ya kutoka katika eneo lake la faraja na kuongeza ufahamu kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na huzuni duniani kote."
"Ujumbe wake ni kwamba hakuna rekodi ambayo ni ya ya kipuzi sana, kubwa sana, au ndogo sana kufikia. Daima kuna nafasi kwa kila mtu na sifa zao za kipekee."
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Israel mwenye furaha alichapisga video ya cheti.
"Rekodi ya Guinness Imethibitishwa," aliandika.
Akiongeza “TUMEFANYA HIVYO! 🎉🔥Tuna furaha kubwa kutangaza kwamba mafanikio yetu ya kuvunja rekodi yametambuliwa rasmi na Guinness World Records! 🎊Ingawa tulikosa barua pepe ya pongezi siku ambayo iliidhinishwa (lo! 🙈), tunalirekebisha sasa kwa pongezi kubwa kwa timu na wafuasi wetu wa ajabu! 🙌Tunajivunia sana kuweka kiwango kipya katika twerking, na hatukuweza kufanya hivyo bila nguvu, shauku na usaidizi wako. Asante kwa kuwa sehemu ya safari hii pamoja nasi! 💖Hapa ni kwa kuvunja vizuizi, kusukuma mipaka, na kutengeneza historia pamoja! 🔥."
Rekodi ya Dunia ya Guinness inahusisha kuorodhesha rekodi za dunia za mafanikio ya binadamu na ukali wa ulimwengu wa asili.