logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya Mulamwah kufichua mtoto wake wa kwanza ambaye mamake aliaga dunia

Ufichuzi huo mpya umewashangaza wengi kwani siku zote watu wamekuwa wakiamini kuwa ana watoto wawili pekee.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani25 July 2024 - 07:13

Muhtasari


  • •Siku ya Jumatano jioni, msanii huyo mwenye umri wa miaka 31 alifichua kuwa ana binti wa miaka saba anayeitwa Lisa.
  • •Ufichuzi huo mpya umewashangaza wengi kwani siku zote watu wamekuwa wakiamini kuwa ana watoto wawili pekee.
amefichua kwamba ana mtoto wa miaka 8.

Ilikuwa mchanganyiko wa hisia kwenye sehemu ya maoni ya chapisho la hivi punde la mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah baada ya yeye kufichua maelezo kuhusu bintiye asiyejulikana.

Siku ya Jumatano jioni, msanii huyo mwenye umri wa miaka 31 alifichua kuwa ana binti wa miaka saba anayeitwa Lisa.

Hata hivyo, zaidi alifichua habari za kusikitisha kwamba mama ya bintiye alifariki kipindi kilichopita.

"Binti yangu mzaliwa wa kwanza, Lisa, mwenye umri wa miaka 7, akielekea miaka 8, tulimpoteza mama yake wakati fulani, lakini ni sawa," Mulamwah alisema kupitia Instagram.

Mulamwah liendelea kueleza kuwa kuna mambo mengi kuhusu maisha yake ambayo watu hawayajui, ambayo baadhi yake atakuwa akiyaweka wazi hivi karibuni ili kuweka mambo wazi na kujibu maswali ambayo watu wanaweza kuwa nayo.

Pia alimhakikishia binti yake kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Upendo mwingi," aliandika chini ya picha ya kumbukumbu yake na Lisa.

Ufichuzi huo mpya umewashangaza wengi kwani siku zote watu wamekuwa wakiamini kuwa mchekeshaji huyo ana watoto wawili pekee, mmoja wa kike ambaye alipata na aliyekuwa mpenzi wake Carrol Sonie na mwingine wa kiume aliyepata na mpenzi wake wa sasa Ruth K.

Binti ya Mulamwah na Sonie, Keilah Oyando, ana umri wa takriban miaka 3 huku mwanawe Oyando Jr almaarufu Kalamwah akiwa na umri wa miezi mitano.

Wanamitandao wamejibu kwa hisia tofauti kufuatia kutambulishwa kwa mtoto wa kwanza wa Mulamwah. Wapo waliomuonyesha sapoti, wengine wakimuonyesha huruma, wengine wameibua maswali huku wengine wakimkosoa mchekeshaji huyo;

Tazama maoni ya baadhi ya wanamtandao;

Anyarsango: You don’t owe the public your private life.

Sheilahsheldone: Let me thank you for bringing her face out to people, it only takes a courageous man to do so, congratulations.

Mrembo_bebi: Nilidhani ni madem tu ndio tunaficha watoto ushago, uyu anafanana ebube the actress yule wa naija

Kdfone_mwenyewe: Na si Ruth aliambia Shosho yakwamba vitukuu wake wote ni wanaume?

Realjackkenya: So for 8 years old child, this is the only photo of her that you have?

Beroobella: Eeeih Baba Lisa, another day to fear konkii


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved