Video ya mwanamume wa Nigeria akivamia kanisa ili kuchukua kwa nguvu mkungu wa ndizi ambao mkewe alikuwa amebeba kwa ajili ya kutoa mchango kwa sasa inavuma kwenye mitandao ya kijamii.
Video hiyo ambayo inanasa matukio ya kushangaza ya wanandoa hao wakipigania ndizi kwenye madhabahu imezua hisia mseto, huku wengi wakitoa maoni yao kuhusu tukio hilo.
Katika video hiyo, mwanamume aliyevalia vmavazi ya buluu anaonekana akiingia kanisani kwa nguvu wakati ibada ikiendelea huku begi kubwa jeupe likiwa limetundikwa mabegani mwake.
Mwanaume huyo ambaye alionekana wazi kuwa na hasira anaonekana akitembea kwa kasi kuelekea madhabahuni ambako anayedaiwa kuwa mkewe alionekana akiwa amebeba ndizi kubwa kwenye begi, tayari kumkabidhi mchungaji
Muda mfupi kabla ya mwanamke huyo kushusha ndizi mgongoni mwake na kumpa mchungaji, mumewe anaonekana akiitoa ndizi hiyo kwenye begi lake na kuondoka nayo.
Mshiriki mwingine wa kike anaonekana akijaribu kukomesha drama hiyo, huku akimpiga mwanamume huyo kwa mikono yake. Mwanamume huyo hata hivyo anafaulu kuchukua ndizi na kuondoka nazo.
Video hiyo imezua hisia mseto huku baadhi ya wanamtandao wakionekana kumuunga mkono mwanaume huyo, wengine wakimkosoa na wengine wakitoa maoni mbalimbali.
Tazama maoni ya baadhi ya wanamtandao;
IRUNNIA: Kwa wale ambao hawaelewi. Mkungu huo wote unagharimu zaidi ya N100,000 na labda mwanamume anakula mara moja kwa siku.
Ikechukwu Kingsley: Alifanya kazi nzuri. Nina hakika hakuna chakula ndani ya nyumba.
Caldril: Mwanaume mwerevu. Kama sijakula, mchungaji hatakula.
Letwin Mandishona: Lol, hiyo ni aibu.
Don-Feran: Nyumbani sio kuzuri na unataka kutoa kanisani.
Thrhymesz: Hata unapomtusi mwanamume huyo, kumbuka tu kwamba Mungu hahitaji ndizi.
JOE X: Mwanaume hajui ni ibada ya kutoa shukrani?
67: Sijui kwa nini wanawake wa Nigeria wanawaheshimu wachungaji wao zaidi ya waume.
Ayila Manase Humble: Yeyote anayejua ladha ya ndizi ya kukaanga lazima afanye kitu kimoja, usicheze!