logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nipe nikupe baina ya Bien na Otile Brown yazuka mtandaoni,wambea mpo?

Bien alidai  kuwa muziki wake ni bora kuliko wa Otile Brown huku akiongeza kuwa ana pesa nyingi kuliko Otile.

image
na Davis Ojiambo

Burudani30 July 2024 - 09:41

Muhtasari


  • •Msanii Bien  alimshtumu Otile Brown kwa kukosoa wimbo wake mpya  aliomshirikisha Prince Indah  na Adenkule.
  • •Otile hata hivyo hakusita alijibu kwa kusema kuwa 'hit song' yake ya mwisho ina umaarufu kuliko ya Bien ya sasa.

Vita vya maneno vimekuwa vikitamba baina ya msanii Otile Brown na Bien kwenye mitandao ya kijamii.

Bien  alimshtumu Otile Brown kwa kukosoa wimbo wake mpya  aliomshirikisha Prince Indah  na Adenkule.

" Otile hakuna pesa uko nayo ...unaongea kama nani?Alitoa Album haikuenda mbali...." Bien alisema.

Hata hivyo Otile Brown hakusita hata kidogo,na kupitia katika ukurasa wake wa Instagram  alidai kuwa hawezi bishana na watu wanaodhani wimbo wowote maarufu ni wimbo mzur(anarejelea wimbo wake Bien)

"Siwezi kubishana na watu wanaodhani wimbo wowote maarufu ni wimbo mzuri na hivyo ndivyo mlivyoharibu mchezo.sasa mnatakiwakutingisha makalio yenu kwenye mitandao ya kijamii kusukuma bidhaa ambayo itaisha tu kwa wiki moja au mbili..." Maandishi yalisomeka kwenye ukurasa wa Insta story wake Otile.

Otile alidai kuwa yeye anaimba  muziki wa asili huku akimponza Bien kwa kusema kuwa alipoteza uhalisia na hivo anaimba muziki ambao watu wanataka.

"...wewe unafanya muziki kwa kundi dogo la watu wa mjini wanaojiona kuwa wanajua maisha sana." 

Aliongeza kwa kusema kuwa Bien aangazie wimbo wake wa mwisho ulio'hit na  wake.Otile alidai kuwa yupo juu na hivo hajaringa wala kwenda kwenye mitandao ya kijamii kushangilia.

"Angalia wimbo wako wa mwisho uliohit na uangalie wangu ,bado ni hit kubwa zaidi nchini kwa upande wa maoni .Bado ni video ya muziki boran zaidi nchini,kwa karib mwaka na sikuhitaji kutingisha kiuno changu kwenye mitandao ya kijamii ,hizi hit mnazosema mko nazo ni gani hizo za maoni milioni 3,milioni 5? Nikifanya hit ni sahihi kabisa  na siyo vitu vya kulazimisha  unavyoshinda mitandao ya kijamii..."

Je,Unahisi ni nani mkali wao kati ya Bien na Otile Brown ?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved