•Chiume alifariki katika hospitali ya Johannesburg Jumanne mchana, taarifa fupi ya familia ilisema.
•Familia iliomba faragha katika kipindi hiki kigumu ikasema kuwa itatoa maelezo zaidi baadaye.
Connie Chiume, mwigizaji mkongwe wa fAfrika Kusini ambaye alikuwa mhusika katika filamu ya Marvel Black Panther, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72, familia yake imetangaza.
Mwigizaji huyo aliyeshinda tuzo nyingi aliigiza katika vipindi kadhaa vya televisheni vya Afrika Kusini vikiwemo Rhythm City, Zone 14 na hivi karibuni zaidi, Gomora.
Chiume alifariki katika hospitali ya Johannesburg Jumanne mchana, taarifa fupi ya familia ilisema.
“Familia ya Chiume inasikitika kuwatangazia kuhusu kuondokewa na mwigizaji maarufu wa kimataifa Connie Chiume,” taarifa hiyo ilisema.
Familia iliomba faragha katika kipindi hiki kigumu ikasema kuwa itatoa maelezo zaidi baadaye.
Mwanawe Nongelo Chiume alikiambia kituo cha runinga cha TV Newzroom Afrika kwamba alikuwa amelazwa hospitali kwa "utaratibu wa matibabu" kabla ya kifo chake.
Chiume aliipamba Televisheni ya Afrika Kusini kwa miongo kadhaa katika vipindi kama vile Rhythm City, huku shirika la utangazaji la nchi hiyo SABC News likimuelezea kama "mnara wa matumaini".
Alipata umaarufu kama mwigizaji mwaka wa 1989 alipotokea katika kipindi maarufu cha televisheni cha Afrika Kusini Inkom’ Edla Yodwa.
Katika filamu ya Black Panther ya 2018, Chiume aliigiza kama Zawavari - mwanachama wa Baraza la jamii ya Wakanda.
Katika muendelezo wa 2022 Black Panther: Wakanda Forever alichukua nafasi ya Zuri (Forest Whitaker) kama Mzee wa Wakanda.
Pia alisherehekewa sana kwa kujumuishwa katika vido ya muziki ya Beyoncé ya Disney iliyotokana na The Lion King, ambayo aliigiza kama mama yake Simba, Sarabi