"Asilimia kubwa ya damu ilikuwa chang'aa, nilishindwa kula" Omosh afunguka kuhusu uraibu wa pombe

Omosh asimulia alivyokuwa mraibu wa pombe na sigara na jinsi alivyofaulu kuviacha

Muhtasari

• Joseph Kamau almaarufu Omosh Kizangila aeleza alivyokuwa mraibu wa pombe na kuvuta sigara na alivyoweza kuacha

Omosh alia baada ya kupoteza kila kitu
Omosh alia baada ya kupoteza kila kitu
Image: instagram

Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahindi High, Omosh Kizangila amefunguka jinsi alijipata ameingia katika uraibu wa vilevi na dawa za kulevya.

Kupitia Obinna TV, Omosh alifunguka kwamba mara ya kwanza alipitisha kinywa chake kwenye chupa ya pombe ni baada ya kumaliza kidato cha nne.

Omosh alifanyiwa mahojiano kwenye Obinna TV na kuweza kueleza alivyokuwa mraibu wa pombe na jinsi alivyofaulu kuiwacha na kuanza upya.

 Joseph Kamau almaarufu Omosh Kizangila anasema alionja pombe pindi tu alipomaliza shule ya upili.

"Kwa maisha, kama kuna mtu anaamua maisha yako ya baadaye si mwalimu,si mzazi ni rafiki...marafiki unaowachagua maishani...hao ndio wanafafanua hatima yako,"Omosh

"Nilikuwa natembea na watu wakubwa..hiyo ndio ilikuwa shida yangu"aliongeza

Kwa maneno yake, ni marafiki zake walimuonyesha kutumia pombe na kuvuta sigara. Alikuwa akizitumia mara kwa mara hasa wikendi mpaka akawa mraibu.

Baada ya kumaliza shule ya upili, Omosh alikuwa kondakta na hapo ndipo alipokuwa akitoa pesa za kununua pombe na dawa za kulevya. Alishindwa kumaliza chuo kwa sababu ya tabia yake ya kunywa pombe.

Alifanyiwa upasuaji kwa sababu pombe ilimuathiri mwili kwa kuwa tayari alikuwa na vidonda vya tumbo (ulcers)

Baada ya yeye kupona alirudi tena kwa unyuwaji kwa pombe sababu ikiwa bado rafiki zake.

Alivyoendelea kuwa maarufu ndivyo alivyoendelea kunywa pombe. Alikuwa akienda bar anakunywa pombe mpaka anazima.

Unywaji wake wa pombe uliathiri kazi yake.

Omosh anasema mwili wake ulikuwa unakubali pombe pekee na hangeweza kula kabla ya yeye kunywa pombe.

Alijaribu kuwacha pombe mara nyingi lakini alishindwa. Kila mara alipokosa kunywa pombe, hangeweza kufanya lolote kwani mwili ulikuwa unatetemeka.

"Asilimia kubwa ya damu yangu ilikuwa chang'aa....singeweza kula kama sijakunywa pombe kwanza" Omosh alisema

Omosh aliweza kuwacha pombe peke yake baada ya kuwa na mkutano kivyake. Sasa hivi ameokoka na hanywi pombe wala kuvuta sigara. Anawashauri vijana wasijihusishe na kunywa pombe kwani madhara yake si mazuri.

Omosh ni mwigizaji wa zamani wa 'Tahidi High' na baba ya wasichana watatu.