logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaharakati Morara Kebaso aanzisha biashara ya kuuza tsheti za chama chake cha INJECT

Alitangaza kwamba tsheti moja itakuwa inauzwa kwa Shilingi 2,500.

image
na MOSES SAGWEarticle.writers[0]?.category

Burudani15 October 2024 - 14:56

Muhtasari


  • Alitangaza kwamba tsheti moja itakuwa inauzwa kwa Shilingi 2,500.
  • “Nguo za INJECT ziko hapa. Ksh 2500 kwa kila moja. Unaweza kuagiza yako mapema,” Kebaso alitangaza.

Mwanaharakati wa kutoa elimu ya kirais, Morara Kebaso ameanzisha biashara ya  kuuza mavazi yenye nembo ya chama chake kipya cha INJECT.

Kebaso, kupiotia kitandazi cha X, aliweka wazi kwamba  ameanza harakati za kukitangaza chama hicho kwa umma cha INJECT, wiki chache baada ya kukisajili rasmi.

"Nguo za INJECT ziko hapa, shili ngi 2500 kwa kila moja,' Kebaso aliandika.

"Nguo hizi zimeundwa ili kuonyesha chapa ya humu nchini Kenya, ubora ni wa kiwango kizuri ndio maana inagharimu 2,500.Pamba safi, UNISEX kwa wanaume na wanawake,' alizipigia debe.

Mwanaharakati huyo alisema kwamba huu ni mkakati wa kukusanya rasilimali zaidi kwa ajili ya kuendesha chama hicho ambacho ni kipya zaidi humu nchini.

"Huu ni mkakati wetu kwa ajili ya kukusanya rasilimali za kuendesha chama. Pesa zote zitatumika katika kujenga harakati zenye nguvu zaidi na shughuli z ufadhili kama vile kesi za mahakama zenye maslahi ya umma," aliongeza.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved