logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chipukeezy akiri kuwa anapendelea ndoa ya wanawake wengi

Mchekeshaji Vincent Muasya almaarufu Chipukeeezy amekiri kuwa anapendelea ndoa ya wake wengi.

image
na Achieng' Kezia

Burudani17 October 2024 - 13:04

Muhtasari


  • Chipukeeezy amekiri kuwa anapendelea ndoa ya wanawake wengi.
  • Amesema amejaribu kuwa mwanafamilia lakini haikufaulu

Mchekeshaji Vincent Muasya almaarufu Chipukeeezy amekiri kuwa anapendelea ndoa ya wake wengi.


Katika mahojiano na Dr Ofweneke, Chipukeezy alisema kuwa yeye haoni uwezekano wake kuwa na mwanamke mmoja.


“Lakini zaidi ninavyozidi kukua na niliyopitia, nilifanya hitimisho kwamba mimi binafsi sidhani kama inawezekana kwangu kuwa na mwanamke mmoja,”alisema


“Nimejaribu kuwa mwanafamilia lakini ilishindikana," aliongeza.


Alipokuwa mdogo, anasema alikuwa anapendelea ndoa ya mwanamke mmoja kwa sababu baba yake na mamake tayari walikuwa wameweka mfano.



“Nilipokuwa mdogo kwa kweli nilikuwa napendelea ndoa ya mwanamke mmoja kwa sababu mfano tayari ulikuwa umewekwa na baba na mama yangu. Wao wamekuwa pamoja tangu wakati huo. Wamefanya harusi, wameoana proper,”



Chipukeezy anasema kuwa amejaribu kuwa mwanafamilia lakini hajafaulu.


“Nimejaribu kuwa mwanafamilia lakini ilishindikana. Tunahitaji mke zaidi ya mmoja. Kweli nilikuwa nimepanga saba lakini sahii niko 3. Naunga mkono mitala,”


Hii sio mara ya kwanza mcheshi huyo kusema kuwa anapendela ndoa ya wake wengi. Hapo awali akwa mahojiano na Mpasho alisema kuwa babu yake alikuwa mume wa wake wengi na yuko tayari kuendeleza urithi wake.


“Pia ninatoka katika familia yenye wake wengi na nimeishi na kufanya hitimisho kwamaba ili niweze kuishi maisha ni nayotaka, ninaamini kuwa mwanamume ni lazima awe na mwanamke zaidi ya mmoja. Haiwezekani kwa mwanamume (inawezekana kwa wengine) lakini wanaume wanafaa kuruhusiwa kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,”



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved