Watengenezaji wa maudhui ya Youtube Mic Cheque podcast wamesitisha shughuli zao za kutengeneza maudhui kwa muda baada ya kifo cha mmoja wa wafanyakazi wake kuaga dunia.
Kupitia ujumbe kwa ukurasa wao wa Instagram, kikundi hicho kimechapisha taarifa hizo za huzuni kikieleza kuwa maudhui ya wiki hii hayatawekwa mtandaoni kupisha maombolezo ya mwenzao aliyefariki.
“Ni kwa mioyo mizito kwamba tunatoa taarifa za kusikitisha. Wiki jana, tulimpoteza mpendwa wetu katika timu ya Mic Cheque Podcast.” Taarifa ya timu ya podikasti hiyo ilisoma.
Kwenye taarifa, timu ya Mic Cheque iliwashukuru mashabiki wake kwa kuelewa kwao na usaidizi wao wakati wa majonzi.
Timu hiyo pia imetangaza kuchukua muda wa wiki moja ili kuomboleza kifo cha mwenzao kikisema kuwa shughuli zao za kawaida zitarejea wiki ijayo.
“Hakutakuwa na vipindi vipya wiki hii tunapochukua muda kutafakari na kukumbuka. Asante kwa kuwa sehemu ya safari hii nasi. Tunaangazia kurejea wiki lijalo.” Wanapodikasti hao walisema kupitia ujumbe kwa taarifa yao.
Hata hivyo, watengenezaji maudhui hao hawakuweka wazi jina
la mwenzao aliyeaga dunia sawia na kutoa taarifa zaidi ya sababu ya mauti
yaliyiotukia wala mipango ya mazishi ya mwendazake.