logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Sijui nisema nini" Akuku Danger aomboleza kwa uchungu kifo cha baba yake

Akuku alizungumzia jinsi mzazi wake huyo aliyekuwa anaugua saratani alivyopigania maisha yake hadi mwisho.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Burudani21 October 2024 - 11:45

Muhtasari


  • Akuku Danger alitangaza habari za kusikitisha za kufariki kwa babake siku ya Jumapili akisema kuwa hali hiyo ilimfanya asijue la kusema.
  •  Sandra Dacha aliungana naye kuomboleza kifo cha babake akisema kwamba alikuwa pia amehuzunishwa na habari hizo.

Mchekeshaji mashuri wa Kenya Mannerson Oduor almaarufu Akuku Danger ameingia katika majonzi kufuatia kifo cha babake.

Akuku Danger alitangaza habari za kusikitisha za kufariki kwa babake siku ya Jumapili akisema kuwa hali hiyo ilimfanya asijue la kusema.

Mchekeshaji huyo alizungumzia jinsi mzazi wake huyo aliyekuwa anaugua saratani alivyopigania maisha yake hadi mwisho na kumtakia heri katika maisha yake yajayo.

“Hata sijui Niseme Nini��������� Nenda Sawa Baba. Familia Yetu Haitakuwa Vilevile Tena. Nakutakia Upitie Salama Hata Unapopitia Awamu Inayofuata. Ng’aa, ulipigana vizuri,” Akuku Danger alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

 Aliambatanisha taarifa yake na picha ya marehemu baba yake.

Rafiki wa karibu wa Akuku, Sandra Dacha aliungana naye kuomboleza kifo cha babake akisema kwamba alikuwa pia amehuzunishwa na habari hizo.

Saratani wewe ni mnyama��� ���, siwezi hata kuelewa kile ambacho wewe (Akuku) unapitia hivi sasa. Nimehuzunishwa sana na habari hizo,” Sandra Dacha alisema.

Mwigizaji huyo alimsifu babake Akuku akibainisha kwamba alikuwa mtu mkarimu ambaye kila mara aliwajali wengine zaidi ya yeye kujijali mwenyewe.

"Baba yako kila wakati alijigamba juu ya jinsi familia yake ni nzuri. Najua ulikuwa na maana kubwa sana kwake. Alikuwa mtu mwema na muungwana wa kweli, kila mara aliweka wengine mbele yake. Bila shaka atakosekana,” alisema.

Aliongeza, Rambirambi zangu zikuletee faraja, na maombi yangu yapunguze maumivu ya msiba huu kuks. @itsakukudanger.”

Kifo cha babake Akuku Danger kinakuja takriban mwaka mmoja baada ya mchekeshaji huyo pia kumpoteza dadake mdogo.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved