Binti Ruto hata hivyo alisema kuwa pengine alipitia msururu wa kuvunjwa moyo kimapenzi kutokana na kwamba aliingia katika uwanja wa mapenzi mapema sana katika maisha yake.
“Nilipokuwa mdogo, nilihimizwa kushirikiana na watu kabla ya kufanya taaluma. Kuwa na urafiki na watu, si lazima kuwa katika uhusiano au kitu chochote, na nadhani kuingia katika mahusiano mapema sana kuliniumiza moyo kwamba ningeweza kuepuka. Si mara mora, mbili au tatu... Sikuwa mvumilivu kufurahia maisha yangu, kuwa mimi bila kuwa mpenzi wa mtu au chochote,” alieleza.
Binti wa Ruto pia alikiri kwamba yeye ni mtoto mtiifu si tu kwa familia yake bali pia kwa kila mtu anayemzunguka, akisema kuwa hicho ndicho kitu anachojivunia zaidi katika maisha yake.
“Nidhamu. Nina nidhamu katika kila kitu ninachofanya au ninachojaribu kuwa, angalau iwe ninafanya kazi, ninakuza uhusiano wangu na Mungu, au kuwa sawa kimwili. Nadhani hilo ni jambo ambalo watu hawalijui kunihusu,” alisema huku akikiri kuwa mpenzi mkubwa zaidi wa chakula cha ugali na dagaa.