logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Mimi nampenda Kim Kardashian, mbona nikimpost mnanishambulia?” – Wema Sepetu

Ziara ya haraka katika ukurasa wake wa Instagram, tulibaini Wema Sepetu alichapisha picha ya mpenzi huyo wa zamani wa rapa Kanye West akiambatanisha tu na jina lake.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani29 October 2024 - 12:02

Muhtasari


  • Ziara ya haraka katika ukurasa wake wa Instagram, tulibaini Wema Sepetu alichapisha picha ya mpenzi huyo wa zamani wa rapa Kanye West akiambatanisha tu na jina lake.

Muigizaji Wema Sepetu amewakaripia kwa kishindo kikuu baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii ambao wameonekana kutokubaliana na hulka yake ya kuchapisha picha za mwanasosholaiti kutoka Marekani, Kim Kardashian.

Kupitia video akiwazomea watu, Sepetu alikiri wazi upendo wake kwa Kim Kardashian akisema kwamba licha ya kutojuana, kila mtu anajua kuwa upendo wake kwa Kardashian si wa kubahatisha au kuazimwa.

Mrembo huyo alisema kwamba ataendelea kuchapisha picha na video za Kim Kardashian hata kama hatowahi mjibu, lakini atawakomoa wanaomtukana.

“Hivi nani asiyejua kwamba mimi nampenda Kim Kardashian hii dunia? Nani asiyejua kwamba mimi nampenda Kim? Kwa nini nikipost picha zake mnania’attack? Hata kama asiponijibu si ni yeye kaamua. Mimi simposti ili anijibu,” Sepetu alisema.

“Mimi nampost kwa mapenzi yangu, mimi sijaanza kumpost Kim leo, jana wala juzi. Nimeanza kumpost Kim kitambo huko na sitoacha kumpost. Kwa sababu sasa mnavyonishambulia hivyo ninapompost ndio mnanichochea nizidi kumpost, nitamposti huyo dada mpaka achanganyikiwe mwenyewe,” aliongeza.

Ziara ya haraka katika ukurasa wake wa Instagram, tulibaini Wema Sepetu alichapisha picha ya mpenzi huyo wa zamani wa rapa Kanye West akiambatanisha tu na jina lake.

Watu wengi katika comment section walimkoromea, wengine wakimwmabia kwamba anajionyesha na hata Kardashian hawezi mjibu wala hamtambui, suala lililomkera kweli Wema Sepetu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved