Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya amedokeza kuhusu mipango ya ndoa aliyokuwa nayo katika siku zake za ujana.
Katika chapisho la Jumanne, mwanasiasa huyo kijana alidokeza kwamba alipanga na kutarajia kuoa kabla ya kufikisha umri wa miaka 26.
Salasya alisema kuwa alikuwa akiomba sana hilo litokee lakini kwa bahati mbaya halikutokea. "Sio kila sala itajibiwa jinsi unavyotaka.
Nilipoomba kushinda 2017, hakuwahi kunijibu, nilipokuwa nikiomba kuoa nikiwa na miaka 26, hakujibu,” Salasya alisema.
Mbunge huyo wa muhula wa kwanza aidha alibainisha kuwa licha ya Mungu kutojibu baadhi ya maombi yake muhimu bado aliendelea kumwamini.
Wiki kadhaa zilizopita, mwanasiasa huyo aliyezingirwa na sarakasi si haba alijaribu kumteka sosholaiti maarufu wa Kenya Huddah Monroe ili kumfanya mpenziwe.
Baada ya wiki nyingi za kumfuatilia kwa dhati mwanasosholaiti Huddah Monroe, mwezi uliopita Salasya hata hivyoalitangaza kuwa hataki tena kufanya hivyo. Katika ujumbe wake, Mbunge huyo wa Mumias Mashariki alidai kwamba juhudi zilizohitajika kumchumbia mrembo huyo ni nyingi mno. Pia aliomba msamaha kwa wasichana wa 'kienyeji' kwa kuwaacha kutafuta malisho ya kijani kibichi.
“Hawa wanaotaka pesa sina uwezo wataishusha Serikali yangu ngoja nirudi kwenye kienyeji wangu, najitenga rasmi na huyu kifaranga, maoni yoyote niliyotoa ambayo yalimuumiza kienyeji changu chochote nje hapa naomba mnisamehe ilikuwa tu mambo ya mitandao ya kijamii.
Mnisamehe nyinyi ndio munawezana na mimi huyu mtu wash wash ndio wako na pesa ya uponyaji,” alisema.
Mbunge huyo alikuwa na misheni kwa muda wa miezi miwili ya kuhakikisha anatafuta njia za kuwavutia Huddah, ili hatimaye wachumbiane naye.
Tamaa yake ilimwona akitoa jumbe nyingi za mapenzi yake kwa msosholaiti huyo, na pia kumnunulia maua.