Ni wazi kuwa mwimbaji na mjasiriamali maarufu Akothee amefanya mabadiliko makubwa kwenye maelezo ya wasifu wake kwenye mtandao wa Instagram.
Ukitazama maelezo ya sasa kwenye akaunti yake ya Instagram, ni dhahiri kwamba mama huyo wa watoto watano ameondoa jina la mume wake Denis Shweizer almaarufu Omosh na badala yake kuweka maelezo ya kazi zake. Hapo awali, alijielezea kama 'Mrs Shweizer' na 'Marketer'.(Muuzaji).
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 hata hivyo sasa amefanya mabadiliko kadhaa kwenye wasifu wake na anajitambulisha kama Mkurugenzi Mtendaji AKOTHEE SAFARIS, Mkurugenzi Mtendaji wa AKOTHEE FOUNDATION na MSHAURI WA MASOKO. Jina Mrs Shweizer halipo tena kwenye wasifu wake wa Instagram.
Aidha, inaonekana pia kwamba mwimbaji huyo mwenye utata tayari amefuta baadhi ya picha za mume huyo wake mzungu ambazo alikuwa amezichapisha katika siku za nyuma.
Akothee alibadilisha wasifu wake wa Instagram mwezi Aprili mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Denis Shweizer katika harusi ya kifahari iliyofanyika jijini Nairobi. Wenzi hao walioonekana kuwa muungano mzuri sana walikuwa wameahidi harusi ya pili ambayo iliratibiwa kufanyika Uswizi lakini haikufanyika.
Hatua ya mwanamuziki huyo kubadilisha tena wasifu wake inajiri wakati anaendelea kuvuma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kukiri kuwa mambo hayajakuwa sawa katika miezi michache iliyopita.
Jumapili jioni, Akothee alitoa taarifa ya kutia wasiwasi kuhusu nyakati za kutisha amepitia katika miezi michache iliyopita.
Mama huyo wa watoto watano alifichua amekuwa akihudhuria vikao vya ushauri maalum vya namtaalamu wa kisaikolojia na kujaribu kupona faraghani kwa miezi miwili iliyopita katika juhudi za kurejesha afya yake ya akili.
Alifichua kwamba masaibu yake yote yalianza baada ya kupata ukweli fulani na maelezo fulani ya kutisha ambayo yalimfanya aingiwe na hofu na kumfanya aingie kwenye dimbwi la mawazo.
"Nimetoka eneo hatari sana na nimekuwa nikipona kwa faragha, niko kwenye mwezi wa pili wa therapy kufuatia kiwewe nilichopitia baada ya kujua ukweli na mambo mabaya ambayo yaliniacha nikitetemeka, Zilipita siku bila chakula. na hakuna kulala, nilihoji na kujijibu mwenyewe, imekuwa nzito sana. Siku zingine, usiku ungekuwa siku na kuniacha mimi nikitazama nje ya dirisha nikikadiria yasiyokuwepo, ningejipata nikitetemeka kwa sababu ambazo siwezi kuelezea, na kumbuka bado nilikuwa na kazi ya kufanya, familia na ufalme wa kulinda. Bado nililazimika kuweka uso mkali na kuwaburudisha mashabiki wangu,” Akothee alisema kwenye kurasa zake.
Aliongeza, "Nelly Oaks amekuwa akipiga simu haraka, akinipigia bila kukoma na alikuwa akiogopa simu yangu ilipokatika, watoto wangu kisawa sawa hasa wasichana tulihakikisha tunaweka timer ili kuangalia kama niko sawa. Rue alinifuata Ulaya kwa hofu. ya kunipoteza, mtoto alinikalisha hadi nikasimama kwa miguu yangu. Nilianza kwa kufuatilia mienendo yangu, niligundua kuwa nilikuwa nikilemewa na hisia mara kwa mara bila sababu, hata mahojiano rahisi tu. Nilikuwa nimekosa utulivu, na sikuweza kuweka kidole juu yake. Sikuwahi kujua kuhusu Unyanyasaji wa Kihisia, hadi nilipoanza matibabu. Nilikuwa katika hali mbaya ya akili iliyonifanya nilipe ksh 50,000 kwa saa kwa kipindi cha saa moja na mtaalamu wa kwanza. Nilikuwa nikitetemeka na kupoteza nguvu, hamu ya kula, usingizi, hofu na hata kupoteza motisha katika kufanya mambo niliyopenda kufanya.”
Akothee alifunga ndoa rasmi na mzungu Dennis Shweizer katika harusi ya kifahari iliyofanyika Aprili mwaka huu baada ya kuchumbiana naye kwa miezi kadhaa. Haijabainika ikiwa wawili hao bado wako pamoja kama mke na mume.