'Alinidanganya anaenda kazi kumbe alikuwa anampeleka dada yangu 'out',Mwanamke asimulia

woman crying.
woman crying.

Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote wapaswa kuwa makini ili moyo wako usiweze kuvunjwa kwa vipande vipende.

Ni mambo ambayo yanatendeka humu nchini, huku mtoto kulala na baba yake au dada kunyakua mpenzi wa dada yake.

Mwanamke mmoja aliwaacha wengi vinywa wazi  baada ya kusimulia jinsi dada yake aliweza kumnyakua mpenzi wake;

"Tulikuwa katika uhusiano na aliyekuwa mpenzi wangu kwa miaka mitano, baada ya kumjulisha kwetu na kupatana na dada yangu alibadilika huku wakati wakuwa nami ukiisha bila ya kujua

Kuna siku moja ambayo aliniambia kuwa anaenda kazi, kumbe alikuwa amempeleka dada yangu out, walionekana na marafiki zangu na kisha wakaniuliza alipokuwa nikawaambia kuwa yuko kazini lakini walikataa na kuniambia kila kitu

Nilipomuuliza alikana kila kitu, baada ya muda niliwapata kitandani knyumbani kwake na dada yangu, sikuwauliza chochote mbali nilienda nilipfika nyumbani nilimwambia mama yangu ambaye alikuwa wa kambo

aliniambia kama siwezi kubali ukweli nimeachwa na mpenzi wangu kwa maana mimi si mrembo kama dada yangu nitoke niende

nilienda na hata leo sina uhusiano wowote na wazazi wangu au dada yangu." Alieleza Mwanamke huyo.

Hukuakiendelea na usmulizi wake alisema kwamba mpenzi wake hakusema chochote kuhusu uhusiano wao bali alimwambia aweze kuendelea na maisha yake.

"Baada ya miaka miwili sijazungumza na familia yangu, wiki jana dada yangu alinipigia simu na kuniambia kuwa ana ujauzito wa ex wangu

nilimpongeza kisha nikamwambia kuwa hasiwahi nipigia simu tena."

Je ni mambo yapi ambayo umepitia katika uhusiano wako wa awali na ambayo hutawahi sahau maishani mwako.