'Mimi ni mali ya mwenyewe,'Millicent Omanga amjibu shabiki aliyemmezea mate

Muhtasari
  • Millicent Omanga amjibu shabiki aliyemmezea mate huku akimwambia kwamba ni mali ya mwenyewe
  • Omanga alisema kwamba hatilii maanani ambacho wakosoaji wake husema
omanga
omanga

Seneta Millicent Omanga huku akiwa na mazungumzo na mashabiki katika sekta ya maswali na majibu alieeleza sababu yake ya kupakia picha huku akionyesha figa yake kwenye mitandao ya kijamii.

Omanga amekuwa akiwasiliana na mashabiki wake kwa njia tofauti.

Mmoja wa mashabiki wake alimuu liza kwanini anapenda kupakia picha zake akionyesha figa yake ilhali yeye ni kiongozi na mama wa kupigiwa mfano na wakenya wengi.

 

Millicent Omanga alichukua fursa hiyo na kumjibu shabiki huyo kwamba,

“Hehe Baraka zingine huezi ficha”.Millicent Alimjibu.

Kwa kawaida lazima kuna wale huwakosesha usingizi kwa ajili ya umbo lake la mwili huku shabiki mmoja akisema kwamba si swali anauliza bali anatamani angemchumbia.

"Si swali lakini natamani ningekuchumbia." Shabiki Alisema.

Kiongozi huyo na mwanasiasa alijibu na kumwambia kwamba amenyakuliwa.

"Hehe mimi ni mali ya mwenyewe”.

Pa Omanga alichukua fursa hiyo na kuwaarifu mashabiki wake kuwa atilii maanani ambacho wakejeli na wakosoaji wake huwa wanasema kumhusu kwa maana anajijua na kujikubali.