Ni rangi ambayo amepaka nywele inaathiri akili yake?Shakilla amshambulia msanii Vivian baada ya kusema haya

Muhtasari
  • Shakilla amshambulia msanii Vivian baada ya kusema kuwa ni mpenzi wa siri wa Mejja
vivian musician
vivian musician

Mwanasosholaiti chipukiza Shakilla anafahamika kwa mambo mengi ambayo amekuwa aitenda na kusema kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi majuzi alimkejeli Mejja kwa kuwa mmoja wa wasanii ambao waliimba kibao cha 'Nairobi' chake msanii Bensoul.

Huku msanii Viviana akitoa maoni yake kuhusu matamshi yake Shakilla alikuwa na haya ya kusema;

 

"Niliona habari mitandaoni kuhusu Shakilla, ambaye alimkejeli Mejja baada ya kibao cha Nairobi kutoka,kati ya wasanii wote ambao walikuwa kwenye kibao hicho aliona Mejja

Ama umempenda kwa siri, kama unataka nikuunganishe naye kuja kwangu Mejja ni rafiki yangu." Vivian Alimwambia mwanasosholaiti huyo.

Baada ya Shakila kuona video yake msanii Vivian alipakia video hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika ujumbe akiwa amempa maneno makali.

"2021 si mitaani mniambia nitafanyia nini huyu, ni rangi ambayo amepaka nywele zake inaathiri akili yake kuwa na ujasiri wa kuniambia hivo

Malkia wa mitaa mimi niwe mpenzi wa siri." Shakilla Aliuliza.

Je drama hii itaendelea mpaka lini?