Bintiye Sonko aonyesha majeraha ya kichapo, mpenziwe seneta Anwar akanusha madai

Muhtasari
  • Seneta wa Lamu Anwar akana madai ya kumchapa mwanawe Sonko
  • Akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba bintiye Sonko ana shida ya akili
  • Haya yanajiri baada ya Saumu kupakia picha akisema kwamba seneta huyo karibu amuue

Bintiye aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Saumu Mbuvi amethibitisha kuvunjika kwa uhusiano wake na Seneta wa Lamu, Anwar Loitiptip.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimjibu mmoja wa mashabiki wake ambaye alikuwa anataka kufahamu iwapo fununu na madai ambayo yanenea wameachana ni kweli.

“Ndio nilitengana naye. Kuna mengi ambayo sijaanika lakini nitawajuza," alisema Saumu. 

 

Saumu pia alichapisha picha ya uso wake uliokuwa umeharibika kupindukia kutokana na kichapo cha mbwa alichopata kutoka kwa Seneta huyo.

saumu.mbuvi (1)
saumu.mbuvi (1)

“Hajawahi kuwa mume wangu. nitawaambia mbona nilimwacha…mwanamume huyo hata hawezi kumshughulikia mwanawe. Nashuku Mungu nilizaliwa hasla. Ni maisha

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo alinifanyia, alikuwa karibu kuniua, maishani mwangu nitapigania haki za wanawake

Usimkubali mwanamume yeyote awe vurugu kwako," Aliongea Saumu.

Huku seneta huyo wa Lamu Anwar akizungumza na Mpasho alikana madai hayo na kusema kwamba mkewe amekuwa na shida ya akili.

Pia alifichua kwamba alimchapa mara moja wakati hakuwa amefahamu kwamba ana shida hiyo.

"Ana shida ya akili ya akili inayoitwa bipolar, ndiyo sababu hatujawahi kukaa pamoja, yeye huvunja vitu, anapiga kelele na kumbukumbu huru kwa hata wiki

 

Ndio lakini mara moja tu kabla ya kujua yeye ana shida ya akili, wito wa familia yake, marafiki, hospitali kila mtu anajua yeye ni mgonjwa .. ni nyinyi tu watu wa vyombo vya habari ambao hamjui na sisi waliamua kujificha ili kulinda jina lake, lakini sasa amegeuza hadithi yake," Anwar Aliambia Mpasho.