Wasanii waliomjibu msanii Bahati baada ya kibao chake cha kejeli

Muhtasari
  • Mapema wiki hii msanii Bahati alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupakia video akivuta sigara
  • Hisia tofauti zilitolewa na wanamitandao huku wengi wakimkejeli kwa tabia yake
  • Baada ya kutoa kibao chake akiwakejeli baadhi ya wasanii wa humu nchini, baadhi yao walitoa hisia tofauti

Mapema wiki hii msanii Bahati alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupakia video akivuta sigara.

Hisia tofauti zilitolewa na wanamitandao huku wengi wakimkejeli kwa tabia yake.

Baada ya kutoa kibao chake akiwakejeli baadhi ya wasanii wa humu nchini, baadhi yao walitoa hisia tofauti, bali awakunyamaza na kungoja wazidi kukejeliwa.

Baadhi ya wasanii ambao walitoa hisia zao na kutoa maoni ni kama vile wafuatao;

1.Ringtone

Msanii au vile hukiita mwenyekiti wa nyimbo za injili alimpongeza Bahati kwa kibao chake kinachofahamika kama 'Fikra za Bahati'.

Pia alimfokea kwa ajili ya kibao hicho, na kumwambia kwamba amemsamehe.

2.Khaligraph Jones

Rappa huyo alimshauri Bahati awache kiherehere kwani hawezi kumfikia mahali alipo, huku akutoa kibao cha kujibu madai yake Bahati.

"Afadhali America Watu si Wakonda Kama Akina @bienaimesol , alafu Naskia @bahatikenya ameanza Bangi na Sigara ameanza Kurap matusi, punguza Iyo Bangi baba wacha Kiherehere. #RESPECTTHEOGS" Aliandika Jones.

3.DK Kwenye Beat

Badala ya kumjibu Bahati kwa maneno alitoa kibao kinacho fahamika 'Bahati wachana na sisi' na kumshauri msanii huyo awachane na wasanii wenzake.