(+Video)Vera Sidika afichua ujauzito wake

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti maarufu Vera Sidika ambaye ni mkewe msanii Brown Mauzo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua ujauzito wake
  • Miezi mitatu iliyopita mnamo Machi, Vera Sidika alikanusha madai hayo ambayo yalienea sana juu ya ujauzito wake
Vera Sidika

Mwanasosholaiti maarufu Vera Sidika ambaye ni mkewe msanii Brown Mauzo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua ujauzito wake.

Baada ya kuwaweka mashabiki wake wakisubiri kwa muda mrefu, amefunua ujauzito wake kwa kusema kuwa ni "Ufunuo Mkubwa."

Alisema kuwa Safari kubwa ya uzazi iko karibu kuanza na kuongeza kwamba anampenda sana mumewe Brown Mauzo.

Miezi mitatu iliyopita mnamo Machi, Vera Sidika alikanusha madai hayo ambayo yalienea sana juu ya ujauzito wake.

Amezungumzia uvumi ambao umekuwa ukifikiriwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba amekuwa akitumia ulinzi.

Vera Sidika anasema kuwa wasichana wengi ambao wanaonekana kama wasio na maadili ndio walio makini zaidi.

Pia aliongezea na kusema kwamba hawezi enda kila mahali akizaa, na mwanamume ambaye anapatana naye.

Hii hapa video ya ufunuo wake;