Mke wa 'Sponsor' wangu ni rafiki yangu-Mwanamke adai

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia vile alipata mke wa 'sponsor' wake ni rafikiye
sad woman
sad woman

Karne hii ya sasa wasichana wengi wameamini lazima wawe katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mzee ili aweze kumkimu.

Asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa wakiwategemea wanaume, licha yao kufahamu kwamba mwanamume huyo ana mke na watoto.

Mwanamke mmoja aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kufichua na kudai kwamba ni rafiki wa karibu wa 'sponsor' wake.

Lakini alimfahamu kabla ya kumpenda mwanamume huyo?

"Mimi nina 'sponsor' ambaye mke wake ni rafiki yangu wa karibu sana, tulipoanza uhusiano wa kimapenzi ndio alinifahamisha kwamba ana familia mke na watoto 2

Lakini sikujua kwamba mke wake alikuwa rafiki yangu wa karibu miaka chache iliyopita, nilijua mke wake ni rafiki yangu baada ya kupatana naye mahali naishi na kuenda kunionyesha mume wake kumbe ni 'sponsor' wangu

Je napaswa kuacha mwanamume huyo kwa maana nilijua mke wake ni rafiki yangu, au niendelee na uhusiano huo," Alieleza mwanamke.