Jamaa mwenye ghadhabu anyoa mrasta aliyekopeshwa nywele na mpenziwe miezi 7 iliyopita

Mdaiwa na ambaye anaonekana dhaifu anasikika akijitetea kuwa hajaweza kulipa deni ile kwani amekuwa mgonjwa kwa muda

Muhtasari

•Mwanaume mmoja mjini Nairobi ameamua kuchukua sheria mkononi baada ya jamaa aliyesukwa nywele aina ya rasta na mpenziwe kukosa kulipia huduma hiyo miezi saba baadae.

•Anapoendelea kutekeleza kitendo hicho, mwanaume huyo anasikika akimuuliza mwenye deni kuhusu malipo ya huduma za mpenzi wake.

Mrasta anyolewa kwa kukosa kulipa deni ya miezi saba
Mrasta anyolewa kwa kukosa kulipa deni ya miezi saba
Image: Hisani

Mwanaume mmoja mjini Kayole, Nairobi ameamua kuchukua sheria mkononi baada ya jamaa aliyesukwa nywele aina ya rasta na mpenziwe kukosa kulipia nywele hizo miezi saba baadae.

Kwenye video ambayo imeenea mitandaoni, mwanaume aliyejawa na ghadhabu anaonekana akikata rasta za mwanaume aliyelazwa chini kwa kutumia makasi.

Anapoendelea kutekeleza kitendo hicho, mwanaume huyo anasikika akimuuliza mwenye deni kuhusu malipo ya rasta alizouziwa na mpenzi wake.

Mdaiwa na ambaye anaonekana dhaifu anasikika akijitetea kuwa hajaweza kulipa deni ile kwani amekuwa mgonjwa kwa muda.

"Nilimwambia namlipa, nimekuwa mgonjwa, si ndio nimerudi" mdaiwa anajitetea.

Hata hivyo kujitetea kwake kunaangulia patupu kwani anayemkata nywele haonekani kushawishika na maneno yake.

Kikundi kidogo cha watu ikiwemo mwanamke aliyemtengeneza nywele jamaa huyo wanasikika wakichachisha kuadhibiwa kwa mdaiwa huyo.

"Miezi saba! Miezi saba Zawadi!" msichana anayeaminika kuwa mdai anasikika akisema.

"Tulikubaliana,nilimwambia kuwa sina kazi.. nilimwambia kuwa nitamlipa sijakuwa kazi" Mdaiwa anaendelea kujitetea. 

Anaonekana kuogopeshwa na tishio la kuchomwa na gurudumu la gari ambalo anapewa na mpenzi wa mdai.

Saa yake inachukuliwa na mwanaume mwingine anayesaidia kumuadhibu.

Tazama video hapa;

Hisani;Mpasho