'Mimi sio 'baby mama' wa mtu yeyote,'Ujumbe wake Anerlisa Muigai uliowaacha wengi wameshangaa

Muhtasari
  • Ujumbe wake Anerlisa Muigai uliowaacha wengi wameshangaa
  • Mwaka huu tu, Arnelisa alithibitisha kuwa anaachana na mumewe Ben pol, na kuwa wanatalikiana jambo ambalo lili washtua wengi kwani wawili hao walionekana wenye mapenzi
Anerlisa Muigai
Image: Maktaba

Mwaka huu tu, Arnelisa alithibitisha kuwa anaachana na mumewe Ben pol, na kuwa wanatalikiana jambo ambalo lili washtua wengi kwani wawili hao walionekana wenye mapenzi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe, akidokeza kwamba kuna jambo kuhusu maisha yake ya uchumba ambayo ynaneda mrama.

"Ukianza kitu, kuwa na ujasiri wa kumaliza pia. NKT. NB, mimi sio mama wa mtoto wa mtu, kwa hivyo usifikirie unaweza kushikilia maisha yangu," Arnelisa aliandika.

Kwa mtazamo wa mambo, Arnelisa anaweza kuwa anazungumzia kesi yake ya talaka na Mwimbaji wa Tanzania Ben Pol, ambaye ni mumewe wa zamani.

Wakati habari za talaka yao zilipoibuka, ilisemekana kwamba Ben Pol ndiye aliyeanzisha taratibu za talaka.

Kupitia kwenye mitandao hiyo Muigai alisema kwamba kile kilihitajika kufanyika kimefanyika na ametia saini.

Alisema kwamba jambo la muhimu maishani mwake sasa ni kazi yake, na amani katika maisha yake.

"Nataka kuweka mambo wazi kuwa nilisaini chochote  kilichohitajika kusainiwa, na sitamani kuhusishwa na mtu yeyote

mtazamo wangu hivi sasa, ni kazi yangu na amani yangu," Aliandika Anerlisa.

Swali ambalo limesalia akilini mwa wanamitandao je kuna shida ambayo imeibuka kati ya Anerlisa na Ben Pol?