'Kama mimi ni maskini basi wewe ni mwizi,'Eric Omondi amjibu Ezekiel Mutua

Muhtasari
  • Hii ni baada ya Ezekiel akiwa kwenye mahojiano, kusema kwamba mchekeshaji Eric anapenda kiki na ni maskini
  • Sio Eric tu pekee bali alisema baadhi ya wachekeshaji ni maskini
Ezekiel Mutua na Erick Omondi
Ezekiel Mutua na Erick Omondi
Image: Hisani

Mzozo kati ya mchekeshaji Eric Omondi na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Uainishaji wa Kenya (KFCB) Ezekiel Mutua umechukua nafasi mbaya baada ya mchekeshaji huyo kumpa ahadi kali Ezekiel.

Hii ni baada ya Ezekiel akiwa kwenye mahojiano, kusema kwamba mchekeshaji Eric anapenda kiki na ni maskini.

Sio Eric tu pekee bali alisema baadhi ya wachekeshaji ni maskini.

Mutua alikuwa ameulizwa kutoa maoni yake, kuhusu Eric baada yake kusema kwamba alimpa Mulamwah shilingi elfu 200,000 ambazo bosi huyo alikuwa ameahidi Mulamwa lakini hakutimiza Ahadi yake.

Eric kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa na haya ya kumwambia Ezekiel;

"Imetosha!!! Lazima tuachane na upuzi !!! Pesa zote ninazopata ni kupitia damu na Jasho, pesa nyingi unayopata ni kupitia Ubadhirifu wa fedha za Umma

Kama mimi ni Maskini basi wewe ni MWIZI, wa PESA za Serikali. Ulimuahidi @mulamwah kujiondoa tu dakika ya mwisho, halafu ukafanya vivyo hivyo na @bahatikenya ili kumshusha tu siku ya hafla yake ilibidi nimpitie kama kaka wa kweli, lakini wewe ni Daktari mwongo

Kwa sasa niko Dar Es Salaam niko karibu kutengeneza HISTORIA kwa kujaza UWANJA WA TAIFA na kupata pesa nikiwa hapo

Ninakuahidi wakati nitakaporudi Kenya nitahakikisha kuwa haushikilii ofisi hiyo ifikapo Septemba, juu huwezi kuita tasnia nzima MASKINI ambao hawajiwezi

Hawa ni Vijana ambao wanajituma ili wapate chakula. INATOSHA !!!" Eric Aliandika.

Je mzozo kati ya wawili hao utaweza kuisha, kwani tumeshuhudia wawili hao wakiwa na vita vya manen mitandaoni.