'...Kwangu kumejaa wababa na proposals,'Mwanawe Akothee,Makadia awaonya wanamitandao wenye tabia hii

Muhtasari
  • Kwa kweli kuwa mtu mashuhuri duniani sio kitu rahisi kwani macho yote yanaelekezwa kwako na wanamitandao
  • Pia kuna wale wanataka kukuharibia jina lako, kwa maana unafahamika sana
Fancy Makadia
Image: Maktaba

Mwanawe msanii Akothee Fancy Makadia kuitia kwenye ukurasa wake wa facebook amewaonya wanamitandao ambao wanamtumia jumbe za kimapenzi.

Kwa kweli kuwa mtu mashuhuri duniani sio kitu rahisi kwani macho yote yanaelekezwa kwako na wanamitandao.

Pia kuna wale wanataka kukuharibia jina lako, kwa maana unafahamika sana.

Makadia hivi majuzi amenza kuonekana kwenye mitandao ya kijamii huku akizungumza na mashabiki wake kwa njia tofauti.

"Kwa hivyo nimegundua baadhi yenu mnauliza juu ya biashara ninazouza au kutangaza Lakini mimi kuishia kuona kuchelewa kwa sababu ya dms nyingi

Nilikuwa naomba ikiwa una maswali yoyote kuhusu biashara unaweza dm au kuwapigia simu, wako katika nafasi nzuri na ya haraka kukuhudumia na kukujibu

Kawaida mimi huwatambulisha na kuacha mawasiliano yao pia. Mimi Huku kwangu kumejaa wababa na proposals," Aliandika Makadia.