Mama mkwe wangu alikuwa anataka kumuua mtoto wangu-Mwanamke asema

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi alipatana na mama mkwe kutoka jehanamu
sad woman
sad woman

Endapo mwanamke ameolewa katika familia ya mpenzi wake ndio itambidi abadili mienendo yake na tabia zake kwani anapatana na watu wenye tabia tofauti na zile za kwao.

Kuna wanawake ambao hupokelewa vyema na kupendwa na wakwe zake, lakini kuna wale hupitia changamoto tofauti.

Nikiwa katika ziara zangu mwanamke mmoja alinisimulia jinsi alipatana na mama mkwe muuaji, ambaye alijaribu kumuua kifungua mimba wake.

"Nilikuwa katika ndoa na aliyekuwa mume wangu kwa miaka 6, tulibarikiwa na watoto 3 lakini kifungua mimba wangu alipitia changamoto nyingi

Mume wangu alimpenda mama yake sana, na kumsikiza, nilitoka katika ndoa hiyo baada ya mume wangu kuambiwa na mama yake anifukuze na akakubali, yaani mume wangu hakuwa na msimamo na wala hangeweza kunitetea

Nilipojifungua kifungua mimba wangu, mama mkwe aliniambia kwamba mjukuu wake sio wa mwanawe kwani hakumfanana 

Ugomvi uliendelea kila kuchao, kuna wakati nilimuachia mtoto wangu nikapata amemwekea sumu, tulipelekana hadi kwa chifu lakini madharau yalikuwa yamefika mwisho

Aliniomba msamaha mikazidi kukaa kwa mume wangu nilidhani mume wangu atabadilika lakini nilikuwa tu naota alinifukuza

KIle naweza kuwahimiza wanaume wanapaswa kuwa na msimamo na kuwaheshimu wake zao,mke wako ni wako na mama yako ni mama yako,"Sylvia Alisimulia.

Je umewahi patana na wakwe wabaya na ulifanya nini ili wakupende?