'Nimechoka kuwapenda watoto wa watu,'Wema Sepetu asema

Muhtasari
  • Wema Sepetu ni muigizaji mashuhuri wa Kitanzania, mjasiriamali wa maduka kadhaa na pia mwenyeji wa kipindi katika programu yake ambayo inaitwa Wema App
  • Wakati huu, ameamua kufunguka juu yake mwenyewe kwenye onyesho
Wema Sepetu
Wema Sepetu

Wema Sepetu ni muigizaji mashuhuri wa Kitanzania, mjasiriamali wa maduka kadhaa na pia mwenyeji wa kipindi katika programu yake ambayo inaitwa Wema App.

Wema kawaida huandaa onyesho la kupikia, ambalo hushiriki na watu mashuhuri wanaopendelea, ambao wanapopika, hushiriki kwenye mazungumzo ambayo  kawaida hufanya wengi kufunguka juu ya mambo mengi.

Wakati huu, ameamua kufunguka juu yake mwenyewe kwenye onyesho.

Ambayo amefichua kwamba amechoka kupenda watoto wa watu wengine, kwa hivyo ameamua kuwa ni bora abaki na mbwa wake Manunu, wakati mwingine ilipotea kwa muda na kwa bahati nzuri akampata tena.

"Nimechoka kuwapenda penda watoto wa watu,sasa nimeona ni heri ni mpate Manunu wangu, Manunu ndiye mtoto wangu sasa nitafanya nini," Alisema Wema.

PIa aliweka wazi kuwa hapendi kukaa pekeyake kwani anaweza jiua

"Kwa hivvyo kuwa pekeyangu katika maisha ni jambo ambalo sipendi kufanya,naweza kuwa pekeyangu siku mkasiki animejiua bure,"