Nataka yoho yangu isukume damu tu-Amber Ray asema baada ya kuthibitisha ameachana na Jimal

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti Amber Ray kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amethibitisha kwamba waliachana na aliyekuwa mpenzi wake Jamal Rohosafi
Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasosholaiti Amber Ray kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amethibitisha kwamba waliachana na aliyekuwa mpenzi wake Jamal Rohosafi.

Katika kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake alisema kwamba yuko 'single' na kwamba kwa sasa moyo wake unasukuma damu.

"Juu sasa uko single una mahitaji gani kutoka kwa mwanamume ambaye unamtaka," Shabiki aliuliza.

Naye mwanasosholaiti huyo alikuwa na haya ya kusema;

"Saa hii nataka roho yangu ifanye ile kazi iliumbiwa kupumb damu tu," Alijibu Amber.

Amber na mkewe Jamal Amira walivuma sana mitandaoni baada ya wawili hao kupigana hadharani.

Pia alisema kwamba hajuti kujuana na Jimal.

"Hapana sijuti kujuana na Jimal ingawa tuna tofauti zetu pamoja, pia kuna kumbukumbu nzuri tumekuwa nazo,"

Pia alisema kwamba atafuta picha za Jimal kutoka kwenye mitando yake ya kijamii, na kuweka wazi kwamba alilia walipoachana.