Zaidi ya wazazi 5 waenda nyumbani kwa Akothee kuomba msaada wa ada ya watoto wao

Muhtasari
  • Zaidi ya wazazi 5 waenda nyumbani kwa Akothee kuomba msaada wa ada ya watoto wao
Msanii Akothee
Image: Instagram

Esther Akoth maarufu Akothee ni msanii ambaye amekuwa akiwasaidia watu ambao hawajiwezi kwa muda sasa.

Huku wanafunzi milioni moja wakitarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza wazazi wengi wamekuwa wakijitahidi ili wawalipie wana wao ada ya shule.

Kuna baadhi yao ambao hawajaweza kutimiza mahitaji ya watoto wao ili kujiunga na shule ya upili kwani walipoteza kazi zao hasa wakati huu wa janga la corona.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee, alifichua kwamba moyo wake umevunjika, baada ya zaidi ya wazazi 5 kutaka msaada wake.

Huu hapa ujumbe wake;

"Huu ni wakati mbaya zaidi wa kuwa nyumbani, kichwa changu kinavunja na moyo wangu umevunjika tayari,eee mayoo zaidi ya wazazi 5 wamo katika lango la nyumba yangu na karatasi za ada ya shule wanalia kama watoto nifanye aje

Mikono yangu imejaa, ni waambie watafute msaada wapi?"Akothee aliandika.