'Mungu akubariki,'Baba yake Diamond amlimbikizia Alikiba sifa

Muhtasari
  • Baba yake Diamond amlimbikizia Alikiba sifa
  • Diamond aliachilia kibao kwa jina IYO siku ya Alhamisi alafu siku moja baadaye Alikiba akawachilia kibao chake Jealous alichoshirikisha mwanamuziki Mayorkun kutoka Nigeria
  • Katika video ambayo imeenea sana mitandaoni mzee Abdul anaonekana akimlimbikizia Alikiba sifa na kusema kwamba kibao chake kimemgusa
Mzee-Abdul
Mzee-Abdul

Huenda mafahari wawili wakubwa wa Bongo Diamond Platnumz na Alikiba wanazozana siku chache tu baada ya wawili hao kuachilia vibao vilivyopokelewa kwa kishindo na mashabiki wao.

Diamond aliachilia kibao kwa jina IYO siku ya Alhamisi alafu siku moja baadaye Alikiba akawachilia kibao chake Jealous alichoshirikisha mwanamuziki Mayorkun kutoka Nigeria.

Katika video ambayo imeenea sana mitandaoni mzee Abdul anaonekana akimlimbikizia Alikiba sifa na kusema kwamba kibao chake kimemgusa.

Mzee Abdul na msanii Diamond hawajakuwa katika uhusiano mzuri kwa muda sasa.

Pia Abdull alimuomba Mungu ampe baraka Alikiba na katika kazi yake ya usanii, kwa muda sasa uvumi umekuwa ukiendelea kwamba wasanii hawa wawili wamekuwa na ugomvi.

"Alikiba  ndugu yangu Mwanangu, shoga wangu nimeipenda nyimbo yako, imenigusa tena sana nafsi yangu, muombe Mungu akuondolee nuksi mbele yako, muziki wako uendelee kaza buti, Alikiba MUngu akubariki sana," Mzee Abdull alizungumza.

Ni ujumbe ambao mashabiki walitoa hisia tofauti na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

isaya_ij: Nenda wasafi uka one alicho fanya mwijaku 😂

djtumbo972: Uyu mzee ajui kuwa kuna kesho 😂😂😂

jowzey_chejjo: Y u getting jealous😂😂😂

jkiba255: King kiba oyeee🔥🔥🔥🔥🔥