'Usijiue na kile hakikupi amani,'Akothee awashauri wanawake wanaowachumbia wazungu

Muhtasari
  • Akothee awashauri wanawake wanaowachumbia wazungu
Msanii Akothee
Image: Instagram

Msanii Esther Akoth maarufu Akothee, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii  ya instagram msanii huyo amewapa ushauri wanawake wa kenya ambao wanawacumbia wapenzi wazungu.

Ushauri wake ulijiri saa chache baada ya mwanablogu mmoja kudai kwamba msanii kutoka mkoa wa pwani  Nyota Ndogo amejitoa uhai baada ya kuachwa na mume wake.

Kama wengi wanavyojua Akothee amekuwa kwenye uhusiano na wazungu, kwa hivyo wanawake hao wanapaswa kufuata ushauri wake.

Nyota alikana madai hayo, na kusema kwamba alimpigia mama yake simu ili asipatwe na mawazo baada ya kuona habari hizo.

"Kwa wanawake ambao wanawachumbia wazungu, mnajua ata mimi nilikuwa huko,usijaribu kujiua na kitu ambacho hakikupi amani, unaeza kuwa na msongo wa mawazo

Nitumie ujumbe kama unahitaji ushauri zaidi,kabla ya kupoteza kichwa chako, au kuenda jela,lakini kumbuka  unamaisha moja chukua uthibiti,"Akothee aliandika.