'Unapiga udaku sana,'Khaligraph Jones amjibu Eric Omondi baada ya ujumbe huu

Muhtasari
  • Khaligraph Jones amjibu Eric Omondi baada ya ujumbe huu

Uhusiano kati ya mchekeshaji Eric Omondi na msanii wa kenya Khaligraph Jones haujakuwa wa kufurahisha kwani wawili hao wamekuwa wakipeana vita vya maneno kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instgram Eric alimtumia msanii huyo ujumbe na kumwambia kwamba anapaswa kuona jinsi anafanya mazoezi licha yake kuacha kwa muda.

Katika ujumbe wake alimuita Jones msichana, baada ya kuona ujumbe wake Msanii huyo alimjibu Eric na kumwambia kwamba wanapaswa kupewa uwanja na washindane.

"Wiki mbili tu kwa Gym na nikama hatujai toka kufanya mazoezi, ambia msichana wangu @Khaligraoh jones natayarisha mbega lake la kulalia," Aliandika Omondi.

Khaligraph jones Alimjibu na kumwambia;

"Si tuweke session Moja Nikuaibishe? Unapiga udaku sana,"

Ugomvi wa wawili hao ulianza pale Eric alikumbuka jinsi Khaligraph alimuinua mbele ya mashabiki wake miaka chache iliyopita na kumtia aibu kwa maana alikuwa na mwili mdogo.