'Mungu amenitimizia furaha yangu,'Aliyekuwa mpenziwe Harmonize, Jacqueline Wolper avishwa pete ya uchumba

Muhtasari
  • Aliyekuwa mpenziwe Harmonize, Jacqueline Wolper avishwa pete ya uchumba
wolper-696x870
wolper-696x870

Aliyekuwa mpenzi wake staa wa bongo Harmonize,Jacqueline Wolper,ana sababu ya kutabasamu baada ya kuvishwa pete yauchumba na mpenzi wake Rich Mitindo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba hamna kitu cha furaha duniani kupendwa na mwanamume ambaye unaempenda.

Pia alisema kwamba Mungu ametimiza furaha yake ya pili baada ya kubarikiwa na mtoto.

"KWA MASHABIKI ZANGU.. hakuna kitu kinaleta furaha kubwa maishani kama kuchumbiwa/kuolewa na mwanaume unaempenda sana MUNGU amenitimizia furaha yangu ya pili baada ya mtoto.....nimeona na kusikia baadhi ya watu wakisema eti nimelia wakati ni pete ya 4 sijui ya 3, yah ni kweli nimelia tena sana maana hata baada ya pale pia nililia sana nyumbani na sababu kubwa za kulia zifuatazo

1:nimevishwa pete na mwanaume nilietokea kumpenda sana duniani

2: Nimevishwa pete na mwanaume alienizalisha kitu ambacho si rahisi kwa maisha ya ujana huu tulionao kwa maana tumekuwa tukizalishwa na kutelekezwa na wengi tunawaona lakini kwangu kuna mwanga tayar juu ya mwanaume huyo

3:Nimevishwa pete katika muda sahihi kwetu pengine pete nilizovishwa awali muda hakuwa sahihi ndio maana hatukuweza kufikia malengo (sio kwa ubaya)

4: sikutegemea kabisa kutokana na story zetu ndani... mara nyingi tulikuwa tunaongelea kuhusu biashara zetu kila siku tufanye nini ili tuweze kuongeza pesa zaidi tufanye nini ili Mtoto wetu P aje akute maisha mazuri zaidi.

Niwaombe mashabiki zangu mzidi kuniombea isiishie kwenye PETE tuπŸ™„πŸ™„πŸ™„ ifike hatua ya "Mimi Jackline masawe nipo tayari kuolewa na Richard ...... kwa raha na shida" 😜😜😜😜😜 huko sasa ndo nitalia week nzima tena nitalia kichaga jamani ....Niko Mapendoni juu ya huyu kijana hapa kiruuuu😒AHSANTENI sana mashabiki zangu," Aliandika Wolper.

Pia alikanusha madai kwamba ni yeye alijinunulia pete ya uchumba na kusema kwamba ana sifa za kupendwa;

"Kuhusu kujinunulia PETE jamani baba P sio mario anaweza kununua pete na pia nina sifa yakupendwa sina sifa yakujitongozesha kwanza nijinunulie pete kwani mimi ndo nilianza kumtongoza jaman! Em acheni kukariri maisha na wala msijali na nyie MTAPENDWA kama MIMI na MTAVISHWA PETE kama ni swala la TIME 😜😜😜😜😜

Mwisho kabisa Asante Nakupenda Baba p ❀️❀️🌹@richmitindo."

Kwa upande wake Rich Mitindo alikuwa na haya ya kusema;

"Upendo ni neno tu mpaka mtu aje na kuupa maana. Upendo wako unatoa picha nzuri ya maana ya mapenzi Ndo maana nikachukua uamuzi huu nimekuchagua na nitakuchagua kila siku za maisha yangu NAKUPENDA @wolperstylish," Aliandika.