'Kosa letu lilikuwa kuacha injili,'Amos na Josh wasema wamerejea,wapeana sababu ya kuachana

Muhtasari
  • Wasanii Amos na Josh wamerejea tena baada ya wawili hao kuachana kwa muda, wawili hao walipendwa na mashabiki baada ya kushiriki katika shindano la Tusker Project Fame 2013
Amos na Josh
Image: Maktaba

Wasanii Amos na Josh wamerejea tena baada ya wawili hao kuachana kwa muda, wawili hao walipendwa na mashabiki baada ya kushiriki katika shindano la Tusker Project Fame 2013.

Wakiwa kwenye mahojiano siku ya JUmatano, Amos na Josh walisema kwamba baada ya kutengana walivunjika moyo,lakini ilikuwa lazima watengane kwa muda.

Wawili hao walitoa vibao kadhaa,moja wapo ikiwa ni;Moto Moto,Baadaye wakimshirikisha KIng Kaka,dansi na mi miongoni mwa vibao vingine.

"Tulikuwa na mkutano, Tulikuwa tumeshauriwa kuamua ikiwa sisi ni wa injili au wa secular

Watu walihisi kama tuko kati, Tulitaka tu kufanya muziki kwani sisi ni wavulana wa kanisa.

Tulisukumwa na vitu vingi na nilikuwa tayari kwa showbiz na nilitafuta biashara ya kichaa na kashfa.

Wakati hauko sawa nguvu yako na jinsi unavyojitolea kwa kitu matone. Tuliamua kwa amani kuachana. "Amos alisema.

Waliongeza na kusema ulikuwa wakati wa kutatanisha kwao.

"Vitu vingi vilikuwa vikitokea na tungeweza kujitosa. Mapumziko yalituumiza.

Watu wanakufuata na unapoacha wanageuza umakini wao kwa kitu kingine. Unaporudi watu hawana hakika ikiwa utakuwa thabiti

Ilikuwa wakati wa kutatanisha sana kwetu kwani tulikuwa tumezoea kuimba kanisani,Sasa uko katika tasnia na kuna mahitaji mengi sana

Kosa letu lilikuwa "kuacha" injili, ilikuwa msingi wetu. Kosa ambalo mimi (Josh) nilifanya ni kwamba niliingia sana kwenye wavu. "

Wawili hao waliwaambia mashabiki wao wamerudi na kuwaomba msamaha.