'Dini huleta mgawanyiko,'Huddah Monroe afichua kwa nini sio wa dini yeyote

Muhtasari
  • Mwasosholaiti mashuhuri Huddah Monroe amezungumzia na kufichua kwamba hana dini yeyote kati ya wakristo na waislamu
  • Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 29 ameeleza kwanini hana dini
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26

Mwasosholaiti mashuhuri Huddah Monroe amezungumzia na kufichua kwamba hana dini yeyote kati ya wakristo na waislamu.

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 29 ameeleza kwanini hana dini.

Kulingana na Huddah dini huleta mgawanyiko kati ya jamii, alisema haya baada ya kusema kwamba kuna baadhi ya mashaiki wake wamekuwa wakimuuliza dini yake.

Pia alisema kwamba hamna Mungu wa wakristo na waislamu , na kuwa MUngu ni mmoja.

"Watu wamekuwa wakiniuliza dini yangu, kusema kweli mimi sio wa dini yeyote,hii ni kwa sababu dini hileta mgawanyiko

Na hauna Mungu wa waislamu wala Mungu wa wakristo, kuna Mungu mmoja naamini Mungu na kile kimeandikwa kwenye biblia na quran," Alisema Huddah.

Huddah amesema kwamba biblia na Quran ni vitabu ambavyo vina hekima, na kwamba watu wanapaswa kushau kile wanafundishwa kwenye makanisa na misikiti, na kuzingatia kile kimeandikwa kwenye vitabu hivyo vitakatifu.