Baba wa mtoto wa Karen Nyamu amwandikia mwanawe ujumbe

Muhtasari
  • Baba wa mtoto wa Karen Nyamu amwandikia mwanawe ujumbe

Mwanawe mwanasiasa Karen Nyamu na mcheza santuri DJ Saint anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo.

Kupitia kwenye ukurasa wake mcheza santuri, wa instagram alimlimbikizia sifa mwanawe na kumtakia heri njema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mapema mwezi huu akiwa kwenye mahojiano na radiojambo, Saint alisema kwamba huwa anamuna mwanawe.

Wawili hao hawaishi pamoja bali wanasaidiana kumlea mwanao wa miaka 7.

"Ninataka kuchukua wakati huu kumtakia siku njema ya kuzaliwa binti yangu mdogo wa kifalme. 'Kukutazama ukikua ni mambo la kufurahisha, yenye athari na ya kushangaza tu. Zaidi ya yote, imekuwa baraka na sehemu ya maana zaidi maishani mwangu. NAKUPENDA SANA na nitajivunia wewe kila wakati. ' heri njema siku yako ya kuazaliwa🥳🥳🥳🕺🕺😘😘," Aliandika Saint.