Jose Chameleon bado amelazwa

Muhtasari

• Chameleon ambaye alizindua ubabe wake katika fani ya muziki kwa ngoma yake ya “Mama Mia” anasemekana kuwa na matatizo ya ini na kongoso.

Staa wa muziki Afrika Mashariki Jose Chameleon
Staa wa muziki Afrika Mashariki Jose Chameleon
Image: TWITTER.COM/JCHAMELEONE/STATUS

Nyota wa muziki raia wa Uganda Jose Cameleon bado amelazwa katika hospitali ya Nakasero nchini Uganda.

Chameleon ambaye alizindua ubabe wake katika fani ya muziki kwa ngoma yake ya “Mama Mia” anasemekana kuwa na matatizo ya ini na kongoso.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Chameleon alipakia picha akiwa hospitalini huku akimshukuru mamake kwa kusimama naye wakati wa magonjwa yake.  

“Asante Mama, Upendo wako uko dhahiri. Hujawahi kukata tamaa juu ya ukweli !!!! Nitakua na nguvu ya kujifunza kutoka kwako. Mungu akujalie uzima zaidi,” Chameleon aliandika.

Mashabiki wengi wa mwanamuziki huyo wamezamia ukurasa wake wa twitter kumtakia afueni ya haraka.

Katika meza ya habari ya Radio Jambo tunamuombea afueni ya haraka Joseph Mayanja maarufu Jose Chameleon.