'Kazi napiga,'DJ Mo na mkewe Size 8 watarajia mtoto wa tatu

Muhtasari
  • DJ Mo na mkewe Size 8 watarajia mtoto wa tatu
Size 8 na DJ Mo
Image: instagram/size 8

Mwanamuziki wa Injili Linet Munyali aka Size 8 Reborn ametangaza kuwa ni mjamzito.

Muimbaji huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitangaza kuwa anatarajia mtoto wao wa tatu namcheza santuri DJ Mo.

Wawili hao walifunga pingu za maisha mnamo Septemba 2013 na tayari wamebarikiwa na watoto wawili ambao wanawasherehekea sana.

Katika chapisho la Instagram akionyesha mtoto wake mapema Ijumaa, Agosti 27, Size 8 alitangaza hadharani na kumshukuru Mungu kwa bidii kwa tunda lingine la tumbo.

"Mungu katika hekima yake amembariki @djmokenya na mimi na mtoto wa 3. Kwa Mungu uwe utukufu," AliandikaSize 8.

Pia DJ Mo alipendezwa na kufurahia habari hizo ambapo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram  alisema kuwa hachezi na kazi.

"Baraka nyingine, Mungu ni mwaminifu mtoto wa tatu,@size8reborn asante  kazi napiga," Mo aliandika.

Hizi hapa jumbe za wanamitandao wakiwapongeza;

wahukagwi: Oh wowww πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ’ƒπŸΏπŸ’ƒπŸΏπŸ’ƒπŸΏπŸ’ƒπŸΏ congratulations guys!!!!!! God is good all the time!

pierramakenaofficial: Oh my!!!! Congratulations!!!!!!!!!

celestinedonkormusic: You two have been busy in front and behind the scenes huh😍

dan_murithi: Nice..God’s blessing to you two