Ata Moi alitawala bila mke,'Gavana Mutua azungumzia kuoa tena

Muhtasari
  • Gavana Mutua azungumzia kuoa tena
  • Mutua alivunja wanawake wengi mioyo, ambao wamekuwa wakimtumia jumbe, baada ya kusema hana haraka ya kuoa
Gavana wa Machakos Alfred Mutua
Image: Instagram

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua amekuwa akivuma baada ya kuachana na mkewe, Lilian Ng'ang'a na baadaye wakaonekana pamoja katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya MUtua.

Wanamitandao na wakenya wengi walidhani kwaba wawili hao waliwadanganya kuwa wameachana lakini akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba wanaishi maisha yao.

Mutua alivunja wanawake wengi mioyo, ambao wamekuwa wakimtumia jumbe, baada ya kusema hana haraka ya kuoa.

Kwenye mahojiano hivi karibuni gavana wa Machakos alitetea uamuzi wake akisema kwamba hata rais wa zamani Moi alikuwa ametawala bila mwanamke wa kwanza.

"Wakati kuonekana kwake kwenye hafla kuliwafanya watu wafikirie kuwa tunapanga kutengana, hatukuwa. Tunaishi maisha yetu. Sasa, nimeulizwa ikiwa watu wanapaswa kutarajia Mke wa Rais mwingine wa Machakos kabla ya kipindi changu kumalizika. Jibu langu ni rahisi: Moi alitawala nchi hii kwa miaka 24 bila Mke wa Rais. "

Alielezea pia kwa nini wawili hao walikuwa wameamua kwenda njia zao tofauti akisema,

"Watu tofauti wanapitia changamoto tofauti katika uhusiano wao, na yangu na ya Lillian haikuwa tofauti. Tofauti pekee ni kwamba tulikuwa na ujasiri wa kutosha kwenda hadharani kuhusu kutengana kwetu."

Baada ya kuulizwa kama angebadilisha jina la hoteli A&L (Alfred & Lillian Hotel) alikuwa na haya ya kusema.

"Kulikuwa na wasiwasi juu ya nini kitatokea kwa jina la hoteli tuliyoijenga pamoja, na ambayo tuliipa jina A & L Hotel. Lakini kwanini nibadilishe jina sasa? Hii bado ni hoteli yetu. Ni mtoto wetu. Wakati wazazi wanaachana, je! wanawanyima watoto wao haki ya kutumia majina kwenye vyeti vya kuzaliwa? " alisema.