'Willy Paul alinilazimisha tufanye ngono bila kondomu,'Msanii Miss P amwaya mtama kwa nini alitoka lebo ya Saldido

Muhtasari
  • Msanii Miss P amwaya mtama kwanini alitoka lebo ya Saldido
Willy Paul na Miss P
Image: Hisani

Msanii wa zamani wa lebo ya Saldido inayomilikiwa na Willy Paul, Miss P amemwaya mtama hasa kwa nini alitoka katika lebo hiyo.

Katika mahojiano ya YouTube na mtangazaji Ali, Miss P alisema Willy Paul alimnajisi mara kadhaa baada ya kuanza vikao vya studio pamoja naye.

"Yeye alinilazimisha kufanya ngono naye, si mara moja si mara mbili. Nilibidi kumwambia mama yangu kwa sababu nilipaswa kupata matibabu.

Nilipaswa kutafuta msaada na mama yangu alinisaidia Alhamdulillah, vinginevyo wakati huu ningekua Nimesha Jifungua au ningekuwa na ujauzito wa miezi tisa." Aliaonge a Miss P.

Aliongeza kuwa alikuwa akipigana na mawazo kuhusu kurudi kwenye lebo ya rekodi au la.

Willy Paul baadaye alikuja nyumbani ili kuzungumza na mama yake na ilikuwa kama makubaliano yalifikia na mambo yaliendelea kama  hamna kitu kilichotokea.

Miezi baadaye hakuweza kuacha na unyanyasaji na hivyo aliacha.

"Sikuweza kuchanganya biashara na radhi. Alikuwa ubinafsi na hakuweza kuniruhusu kufanya kazi na wasanii wengine wa kiume

NIlikuwa nimesaini mkataba wa miaka tano, lakini nilipotaka kutoka nilihusisha wakili wangu ili waniwachilie

Mimi sijali kile watu watasema, niliogopa kujitokeza mapema kwani nilikuwa naona Paul ni msanii ambaye anajulikana sana."

Miss P aliwahidi mashabiki wake kwamba ataendelea kutoa vibao, huku akisema kwamba yuko tayari kufanya collabo na wasanii wengine.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

#PresenterAli