'Baba yangu wa kambo hakutukubali mimi na dada yangu,'Mwanahabari Salim Swaleh afichua haya kuhusu maisha yake

Muhtasari
  • Mwanahabari Salim Swaleh afichua haya kuhusu maisha yake
  • kizungumza wakati wa mahojiano na Churchill Swaleh alisema wanawake wa Irani hawana utii
Salim Swaleh
Image: Maktaba

Mwanahabari wa runinga ya NTV Salim Swaleh anasema aliamua kurudi na kupata mke nchini Kenya licha ya kuishi nchini Iran kwa miaka 6.

kizungumza wakati wa mahojiano na Churchill Swaleh alisema wanawake wa Irani hawana utii. 

"Mahari ya wasichana wa Kiajemi ni ghali sana. Wanasimama juu ya kiwango cha uzito na kukuambia kuwa 1/4 ya uzito wao katika dhahabu na ndivyo unapaswa kuwapa 

PIa wamewafanya wanaume wakaliwa, kwani katika sheria yao inasema kwamba ukimuacha mwanamkke wako pia unapaswa kulipa mahari

Wanaume wa Irani pia wana wivu sana wakati wanapoona mtu wa kigeni na wanawake wao. Wanaweza kukupiga kwa urahisi," Alisema Swaleh.

Swalim Swaleh anasema ilikuwa kazi ngumu kwa baba yake wa kambo  kumkubali yeye na dada yake.

Hii ilikuwa baada ya kuolewa  kwa mama wa Swaleh baada ya baba yake mzazi kuaga dunia.

"Mama yangu alirudi na kuolewa tena. Mtu huyo hakutaka kukubali dada yangu na mimi, alitaka tu mama yangu. Ilichukua mengi ya kumshawishi kutukubali."