'Ishi na mwanamume huyo kulingana na jitihada zake na msimamo,'Zari Hassan awashauri wanawake kuhusu uhusiano wa kimapenzi

Muhtasari
  • Zari Hassan awashauri wanawake kuhusu uhusiano wa kimapenzi
Zari Hassan
Image: Maktaba

Mwanasosholaiti kutoka Uganda na baby mama wa msanii Diamond  Platnumz  anaweza kuwa 'single', lakini hiyo haimzuii kuwashauri mashabiki wake kuhusu uhusiano.

Zari hivi karibuni alishiriki maoni yake juu ya jinsi wanawake wanapaswa kuishi kwa wanaume katika maisha yao.

Aliwashauri kuwatendea kulingana na nishati wanazozipa.

 'Sis ishi na mwanamume huyo kulingana na jitihada zake na msimamo' aliandika Zari.

Mwezi uliopita, Zari aliambia shabiki ambaye aliuliza juu ya hali yake ya uhusiano kwamba yeye hana mchumba na wala hatarajii wala hatafuti mchumba.

Alifchua haya Awiki chache baada yakudai kwamba hachumbiani na mpenziwe wa awali, ambaye alimtambulisha kwa mashabiki siku ya wapendanao mwaka huu.

Kwa mujibu wa Zari, alipaswa kumruhusu aende kwa sababu hawakujengana kwa njia yeyote.

Pia mwanasosholaiti huyo alifuta picha zote ambazonalikuwa amepakia kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mpenzi wake.

Zari siku mbili zilizopita aliwapongeza wanawake a,bao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kujikimu na hata kulinda familia zao.